Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John
Pombe Magufuli amesema kuwa wamekubaliana na Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco kujenga Uwanja wa Mpira wa miguu wa
kisasa mkoani Dodoma utakaogharimu dola
milioni 100.
Rais Magufuli ameyasema hayo jana Ikulu Jijini Dar es
Salaam baada ya kutiliana saini kwa mikataba 21 ya makubaliano ya ushirikiano
kati ya nchi za Tanzania na Morocco.
“Mbali na mikataba baina ya Tanzania na Morocco nimezungumza
mambo mbalimbali na Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco na nimemuomba atujengee Uwanja
mkubwa wa mpira pale Makao Makuu yetu Dodoma utakaokuwa na thamani kati ya dola
milioni 80 hadi 100 na amesema ataujenga,
kwa hiyo utakuwa Uwanja mkubwa kuliko wa Dar es Salaam”. Alisema Rais Magufuli.
Mbali na hayo Rais Magufuli amewahakikishia
wafanyabiashara wa Morocco kuwa Tanzania ni salama na inapenda kushirikiana nao,
na kuwa nchi yetu iko katika mwelekeo mzuri wa uwekezaji ambapo uchumi wa nchi
yetu unategemea kukua kwa asilimia 7.2 mwishoni mwa mwaka.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw.Salahddine
Mezour ameishukuru nchi ya Tanzania kwa ushirikiano iliounyesha na kusema kuwa
Morocco itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali kwa kuwa
ina utulivu wa kisiasa na icho ndo kimekuwa kivutio kikubwa katika kuwekeza
kwao nchini hapa.
Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco yuko nchini kwa
ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais, Dk John Pombe Magufuli ikiwa
na lengo la kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili na kutiliana
saini mikataba 21 ya makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
No comments:
Post a Comment