Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe.January Makamba ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika
ziara yake Waziri Makamba ameshuhudia uharibifumkubwa wa mazingira hususan
pembezoni mwa ziwa Rukwa.
Waziri Makamba amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha Nankanga kwamba
mwaka 2000 kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka
2016 chanzo hicho kimepungua hadi kufikia mita tatu.
“Tafiti zinaonyesha kuwa
kupungua kwa kina hicho pamoja na mambo mengine kunasababishwa na kilimo cha
milimani na kandokando ya ziwa, na ulishajiwa mifugo katika Vyanzo vya maji,” Makamba alibainisha.
Katika ziara yake baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi
hicho, Waziri Makamba ameazimia kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo
mahsusi kwa mazingira na kanuni za matumizi ya maeneo hayo zitaandaliwa
ilikunusuru Ziwa Rukwa.
Pia, wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa
kutenga pesa zitokanazo na tozo mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa
alama maalumu ‘beacons’ ili kuainisha eneo tengefu na kuagiza kuwazoezi hili
lifanyike haraka.
Aidha, Mhe. Makamba amesisitiza juu ya upandaji wa miti na
ameonyesha masikitiko yake kwa Mkoa wa Rukwa kuwa na upungufu wa miti ya asili
na ile ya kupanda kwa kiwango kikubwa. “nimetembea zaidi ya kilomita 200
sijaona miti iliyopandwa,” Makamba aliongezea.
Wakazi wa Mkoa wa Rukwa wamefahamishwa na kusisitizwa kuwa
kuanzia mwakani itakuwa lazima kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari
kuripoti na miti na kutakiwa kuitunza mpaka pale watakapomaliza shule. Waziri
Makamba ameahidi kuleta wataalamu na kutoa orodha ya miche inayostawi katika
kila kijiiji ili kurahisisha uoteshaji wa miti.
Katika hatua nyingine, Waziri Makamba amekutana na viongozi
mbalimbali wa dini na wazee wa Mkoa wa Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya
Amani,na kuahidi kugharamia Mkutano wa kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo
nakusisitiza agenda ya mazingira iwepo.
Mkoani Rukwa Waziri Makamba ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na
kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo na Mkutano wa Hadhara katika
No comments:
Post a Comment