Wednesday, 5 October 2016

BEI ZA MAFUTA KWA MWEZI OKTOBA ZASHUKA

















Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji Tanzania, (EWURA), wametangaza bei mpya za kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli nchini kwa mwezi Oktoba ambazo zimepungua kulinganishwa na za mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo amesema ni muhimu wauzaji wa mafuta wakatambua bei hizo mpya za kikomo ili kuepusha misuguano.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo imesema kuwa sababu kubwa ya kushuka kwa bei hizo za mafuta aina ya petrol, dizeli na mafuta ya taa inatoka na kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia.
Aidha Ewura imesema kuwa itaendeklea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta ikiwa na lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

Bei za mafuta ya Petrol, Dizeli, na mafuta ya taa zimebadilika ikilinganishwa na tolea la tarehe 7 Septemba ambapo kwa mwezi Oktoba Bei ya petroli imepungua kwa shilingi 12 sawa na asilimia 0.66, dizeli kwa shilingi 48 sawa na asilimia 2.76 na mafuta ya taa kwa shilingi 15 sawa na asilimia 0.91.


No comments:

Post a Comment