Shule ya msingi Butwa iliyopo
katika kijiji hicho ndani ya kisiwa cha Izumacheli ziwa Victoria upande
wa Wilaya ya Geita inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu wanawake, jambo
ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike.
Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1983 na sasa ina umri wa miaka 33 ikiwa ni
shule ya pili katika kata ya Izumacheli, imefahamika kuwa walimu wa jinsia hiyo
wanapopangiwa kuripoti maeneo hayo wamekuwa waonga wa kuishi kutokana na
mazingira kuwa magumu kwao.
Leticia Zakayo ni mwanafunzi darasa la sita, ni msichana pekee
aliyethubutu kupaza sauti yake kwa niaba ya wenzake akiiomba serikali kutatua
changamoto ya walimu wa kike shuleni hapo.
‘’Mimi ni mwanafunzi wa darasa la sita tangu nianze masomo yangu shuleni
hapa sijawahi kumuona mwalimu wa kike..watoto wa kike tunakabiliwa na
changamoto nyingi sana mmoja wetu anapougua tunashindwa kuwaelezea matatizo
yetu hawa walimu wa kiume…kama mnavyojua tunakabiliwa na changamoto
nyingi,’’alisema Leticia zakayo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Omary Shabani aliangazia changamoto
zinazowakabili watoto, ambapo alisema kuwa mtoto wa kike anapopata matatizo
wamekuwa na utaratibu wa kusaidiana wao kwa wao.
“Ni kweli changamoto hii imekuwepo kwa muda mrefu ni wakati wa
serikali kulitizama hili kwa mapana yake watoto hawa hawako huru sana pindi
wanapopatwa na shida, wanapokumbana na changamoto tumekuwa tukiwatafuta
wanafunzi wakubwa wanasaidiana,’’alisea mwalimu Mkuu.
Mwalimu Herman Kapufi ni mkuu wa Wilaya ya Geita wa kwanza kuitembelea
shule hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 33 iliyopita ambapo katika ziara yake
alipoitembelea jana alikumbana na changamoto hiyo na kuahidi kuwa kufikia
januari mwakani shule hiyo itakuwa na walimu wa kike.
No comments:
Post a Comment