Kwa mujibu wa Benki ya
Dunia ripoti inasema kuwa, idadi ya watu masikini sana imepungua kwa zaidi
ya watu milioni 100 licha ya kwamba uchumi wa dunia unakuwa kwa kusua sua.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka Benki ya Dunia,
mwaka 2013 karibu watu milioni 767 walikuwa wanaishi kwa pato la dola 1.90 kwa
siku wakati mwaka 2012 idadi ya watu masikini sana ilikuwa ni milioni
881 kote ulimwenguni.
Ripoti hiyo pia imeonesha
kuwa, mwaka 2013 idadi ya watu masikini zaidi ilipungua kwa karibu
watu bilioni moja na milioni mia moja ikilinganishwa na mwaka 1990 licha ya
idadi ya watu kuongezeka duniani huku ikieleza kuongezeka kwa misaada kwa
watu masikini duniani.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa, dunia imekaribia kufikia malengo
yaliyokusudiwa na Umoja wa Mataifa ya kupunguza umaskini kwa kiwango
kikubwa ifikapo mwaka 2030.
No comments:
Post a Comment