Saturday 4 June 2016

PICHA:MAMA JANET MAGUFULI AKITOA MSAADA MKOANI LINDI KWA WATU WASIOJIWEZA







































Wananchi wa Kijiji cha Nandagwa Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wakimlaki Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa kwa ajili ya Kambi ya Wazee ya Nandanga iliyopo katika kijiji hicho.



Mratibu wa kambi ya Kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga Bw. Agnerus Chiamba akimpa maelezo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kuhusu nyumba za malazi katika kambi hiyo, aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa.


Baadhi ya Vitu vilivyotolewa kwa ajili msaada katika kambi ya kulea Wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga.




Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.



Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi na kuahidi kuendelea kusaidia kambi hizo za wazee na watu wenye ulemavu wa ukoma ambapo mpaka sasa meshatoa msaada katika kambi 4 katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Lindi na Mtwara yenye thamani ya Takribani shilingi 250.



Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiagana na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi baada ya kutoa msaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo eneo hilo.

No comments:

Post a Comment