Saturday 18 June 2016

SPAIN TIMU YA KWANZA KUFUNGA MABAO MENGI EURO 2016



Mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la Mataifa ya Ulaya timu ya taifa ya Hispania imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora baada ya kuichapa Uturuki kwa bao 3-0 kwenye mji wa Nice, Ufaransa.

Wakionesha kiwango cha juu kwenye michuano, Spain wamekuwa timu ya kwanza kufunga magoli zaidi ya mawili kwenye mechi za michuano ya Euro 2016.
Alvaro Morata aliifungia bao Spain kwa kichwa kisha Nolito akaongeza bao lingine kwa shuti kali la karibu.
Goli la tatu lilipatikana baada ya kupigwa pasi 21 likijumuisha wachezaji tisa kisha Morata akaweka mpira kwenye neti.
Spain kwenye ubora wao
Spain waliingia kwenye mchezo wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wao wa ufunguzi wa michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008 wakati Uturuki wakiwa wanakosolewa kwa kiwango chao duni kwenye mchezo waliopoteza dhiudi ya Croatia na mchezo wao dhidi ya Spain ukamalizika kama wengi walivyotarajia.
Kikosi cha Hispania hakijapoteza mchezo dhidi ya Uturuki kwa miaka 62 sasa huku wakiwa hawajafungwa katika mechi 13 zilizopita kwenye fainali za kombe la Ulaya, walitawala mchezo na walikuwa hawazuiliki.
Gerard Pique na Nolito, walikaribia kufunga kabla ya mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata kuunganisha kwa kichwa krosi ya Nolito na kuipatia bao Spain.
Turan azomewa na mashabiki wake
Kikosi cha Fatih Terim kimekuwa kikikosolewa pamoja na star wake Arda Turan baada ya kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wao wa ufunguzi na huenda mambo yakawa mabaya zaidi baada ya kipigo kingine kutoka kwa Spain.
Kipindi cha pili mashabiki wa Uturuki walimzomea kiungo wao na klabu ya Barcelona baada ya star huyo kupooza shambulizi la counter-attack lakini nyota huyo alijibu mapigo kwa kuwaonesha dole gumba.
Mashindano haya ni machungu kwa Turan ambaye alinunuliwa na Barcelona kwa ada ya euro milioni 40 akitokea Atletico Madrid lakini alijikuta akizomewa na mashabiki wa taifa lake tangu mchezo dhidi ya Croatia.
Dondooo muhimu
Kadi ya njano aliyooneshwa Sergio Ramos sekunde ya 58, imekuwa kadi ya mapema zaidi kwenye michuano ya Euro tangu Aleksandrs Isakovs kwenye mchezo wa Latvia dhidi ya Germany sekunde ya 40, ilikuwa mwaka 2004.
Nolito amekuwa mchezaji wa sita tofauti wa Spain kwenye historia ya michuano ya Euro kufunga na ku-assist kwenye mchezo mmoja akiungana na Pereda, Cesc Fabregas, Dani Guiza, David Silva pamoja na Fernando Torres.

Uturuki hawajapata clean sheet kwenye michuano ya Euro tangu waliposhinda 2-0 dhidi ya Belgium kwenye michuano hiyo mwaka 2000, wamefungwa magoli 15 kwenye mechi nane tangu wakati huo.

Morata anakuwa mchezaji wa tano kufunga kuanzia magoli mawili kwenye michuano ya Euro akiwa kwenye timu ya taifa na kuungana na Alfonso Perez, David Villa (hat-trick v Russia), Fernando Torres and Xabi Alonso.

Spain hawajapoteza mechi kwenye michezo yao 14 ya michuano ya Euro (W11 D3), huku wakiwa hawajaruhusu goli ndani ya dakika 690


No comments:

Post a Comment