Tuesday 7 June 2016

RAIS JOHN MAGUFULI AMTEUA JAJI FERDINAND WAMBALI KUWA JAJI KIONGOZI




Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani Dkt.John Pombe Magufuli leo 07 June 2016 amemteua Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa jaji Kiongozi.

Jaji Ferdinand Wambali anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Shaaban Ally Lila aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mkoani Tanga.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 June, 2016.

No comments:

Post a Comment