Monday 13 June 2016

MKUU WA MKOA WA GEITA AWATAKA WADAU WA SEKTA YA USAFIRI KUFUATA UTARATIBU WAKATI WA KUTOA HUDUMA KWA UMMA


Mkuu wa mkoa  wa Geita meja jenerali mstafu  Ezekiel Kyunga amewataka wadau wa sekta ya usafiri wa umma kuakikisha wanafuata   taratibu na sheria pindi wanapokuwa wakitoa huduma kwa umma.


Akizungumza hivi karibuni katika semina ya wadau wa sekta hiyo,Kyunga,amesema kuwa wakazi wengi mkoani hapa wamekuwa wakitumia usafiri wa umma,lakini bado kumeonekana kuwepo kwa changamoto  na miongoni mwa changamoto hizo ni wamiliki kushindwa kuelewa taratibu zilizolewa na mamlaka ya usafiri nchini Sumatra.

Aidha kwa upande wake,afisa sheria mkuu mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu na majini Sumatra,Leticia Mtaki,amesema kuwa kwa sekta ya upande wa bara bara wamekuwa na changamoto nyingi na kubwa zaidi ni kutokana na miundo mbinu na baadhi ya watoa huduma kutokuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.

Mtaki,amewaomba  watoa huduma kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria za usalama barabara lengo ikiwa ni kudhibiti ajali ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.


No comments:

Post a Comment