Saturday 18 June 2016

WATOTO WENYE UMRI WA MWAKA 1 NA MIEZI 7 WAFUNGIWA NDANI KISHA MAMA YAO KWENDA KUNYWA POMBE

Ikiwa  ni siku chache tangu kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika imebainika vitendo vya ukatili dhidi ya watoto bado ni tatizo katika jamii nzetu ambapo katika mtaa wa Msalala road  kata ya Kalangalala ,mkoani hapa mama anayejulikana kwa jina la Janeth Yohana, amekuwa akiwafungia ndani watoto wenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba  ambao ni mapacha na yeye kwenda katika vilabu vya pombe za kienyeji.


Storm habari ilifanikiwa kufika katika mtaa huo na kuona mazingira ambayo wanaishi watoto hao kuwa si mazingira ya kuridhisha kwani ndani kulikuwa ni kuchafu na watoto wakiwa katika hali ya upweke na simazi.hata hivyo baadhi ya majirani wamesema kuwa ni desturi na tabia ya mama huyo kuwaacha watoto hao na kwamba walisha wahi kumshauri mama huyo lakini amekuwa ni mgumu wa kuelewa.

Aidha kwa upande wake diwani wa kata ya Kalangalala,Sospeter Mahushi,amesema kuwa kuhusu tuhuma za kufungiwa ndani watoto hao hakuwa nazo mpaka pale alipotafutwa na mwandishi wetu na kwamba maamuzi ambayo atayafanya atamwagiza mtendaji aweze kuwakamata wazazi wa watoto hao huku wakishughulikia njia ambavyo wanaweza kuwatafutia namna ya kuwatunza watoto hao.

Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida mama huyo huwa anapokea pesa za ruzuku ambazo ni za TASAF,na amekiri kupokea fedha hizo na kwamba pindi anapopokea huwa ananunulia mahitaji ya nyumbani na mpaka sasa ni awamu nne amekwisha kupokea.


Hadi Storm habari inaondoka eneo la tukio iliacha watoto hao wamechukuliwa na msamalia ambae alikuwa ni jirani wa mama huyo huku mama huyo akipelekwa katika dawati la jinsia lililipo kituo cha polisi.

No comments:

Post a Comment