Wednesday 15 June 2016

KIWANDA CHA NYAMA MKOANI SHINYANGA CHATELEKEZWA-STEVEN MASELE


Mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Masele 

Hayo yameelezwa na Mbunge wa Shinyanga Mjini Steven Masele na kutaka kauli ya serikali juu ya kukichukua kiwanda hicho kutoka kwa mwekezaji na kuruhusu wananchi kulima eneo la kiwanda hadi hapo serikali itakapotatua tatizo la kiwanda hicho kwani ahadi ya kukifufua ni ya miaka mingi.

Akijibu swali hilo Waziri wa Viwanda Uchukuzi na Uwekezaji Charles Mwijage amesema kwamba serikali inapitia viwanda 55 ambapo serikali imewataka waliobinafsishiwa viwanda kuandika andiko la kibishara ili kuonyesha uwezo wao wa kuvifufua na kuajiri na wakishindwa kufanya hivyo kwa muda waliopewa serikali itavitwaa viwanda hivyo kikiwemo kiwanda cha nyama Shinyanga.


Aidha kuhusu kuwapa wananchi wanaozunguka eneo la kiwanda kupewa eneo la kulima hadi kitakapoanza kiwanda Waziri Mwijage amesema kwamba wananchi wasiguse maeneo hayo ili mwekezaji asije kupata kigezo cha kutofufua kiwanda hicho alichowekeza kisheria.

No comments:

Post a Comment