Monday 6 June 2016

WANANCHI MKOANI GEITA WATAKIWA KUWEKEZA MALI ZAO MKOANI HAPA

Mkuu wa mkoa wa Geita,mh Ezekiel  Kyunga,amewataka wananchi na wazawa wa mkoani hapa kujenga destuli ya kuwekeza katika maendeleo na kuacha destuli ya kuwekeza nje ya mkoa.

Wito huo ameutoa katika uzinduzi wa hospatali ya Makoye  wakati alipokuwa ni mgeni rasimi,amesema kuwa kwa sasa Geita ni mkoa na sio wilaya kama ilivyokuwa hapo zamani hivyo ni vyema kwa wazawa na wananchi wa maeneo mengine kuja na kuwekeza miradi ya maendeleo  mkoani hapa.

Aidha mkuu wa mkoa,ameongeza kuwa kutokana na ugomvi ambao umeendelea kuwepo baina ya wafugaji na serikali ni vyema kwa wafugaji kuona busara ya kuuza mifugo yao na kuwekeza katika shughuli zingine  ambazo zitaleta tija kwa jamii.

Kwa upande wake  mkurugenzi wa hospitali hiyo,Makoye Othuman,amewataka waandishi wa habari kuendelea kuutangaza mkoa wa Geita,na kuwaelimisha wananchi juu ya athari za miamba taka maarufu kwa jina la magwangala kuwa hayana faida kwa mkoa kwani wale ambao wanang’ang’ania  ni watu ambao wanakuwa wanauhujumu mgodi.


Wananchi ambao wamefika katika uzinduzi wa hospatali hiyo wamepongeza kwa juhudi ambazo zimefanyika huku wakiamini kuwa huduma zitakazo tolewa zitakuwa  ni za uhakika.

No comments:

Post a Comment