Tuesday 7 June 2016

POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA WAFUASI WA CHADEMA


Polisi Wilayani Kahama wametumia mabomu ya machozi kutawanya makundi ya wananchi wanaokutwa wamekusanyika katika maeneo mbalimbali.

Mabomu hayo yameendelea kurindima katika viwanja vya CDT ili kuwatawanya wananchi hao waliokusanyika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara wa Chadema.

Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo kuanzia saa 9.00 alasiri kabla ya polisi kuupiga marufuku na jeshi hilo kuzuia mikutano mingine kama hiyo nchini.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni la leo na Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato Mssanzya amepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadharahadi hali ya usalama itakapotengemaa.

Amesema Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yoyote au chama chochote kitakachokaidi agizo hilo.

No comments:

Post a Comment