Friday 17 June 2016

WAZAZI NA WALEZI MKOANI GEITA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI KATIKA KUKOMESHA VITENDO VYA KIKATILI KWA WATOTO


  
Kutokana na kuwepo kwa vitendo vingi vya ukatili kwa watoto kama kupigwa kulawitiwa na kubakwa, wazazi na walezi mkoani Geita wametakiwa kushirikiana na viongozi mbali mbali ikiwemo polisi katika kuhakikisha hali hiyo inatokomezwa.

Kauli hiyo imetolewa na afisa tawala wa halmashauri ya wilaya ya Geita bi  Janeth Mobe alipokuwa akitoa hotuba kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya geita mh Manzie Omary Manguchie ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto afrika yaliyofanyika katika kijiji cha Lwamgasa kilichopo wilayani na mkoani hapa.

Amesema kuwa jamii inatakiwa kushirikiana kwa pamoja katika kutokomeza vitendo hivyo huku akilitaka jeshi la polisi kuongeza doria na kwamba watuhumia wanaokamatwa kwa makosa hayo sheria ichukue mkondo wake ili kokomesha hali hiyo.

Ameongeza kuwa halmashauri ya wilaya ya Geita inazo kesi  66 zilizoripotiwa kuanzia julai 2015 hadi june 2016 ambapo kesi za ubakaji ni 52 na ulawiti ni 2 na kwa sasa kesi hizo ziko mahakamiani huku kesi 37 ziko katika upelelezi.

Kwa upande wao watoto waliohudhuria katika maadhimisho hayo wameipongeza serikali kwa hatua ambazo imekuwa ikichukua huku wakiiomba serikali kuendelea kukomesha hali hiyo kwa kuwafikisha mahakamani wale wote wanaobainika kujihusihwa na vitendo viovu kwa watoto ili iwe fundisho kwa watu wengine.


No comments:

Post a Comment