Monday 13 June 2016

WANANCHI MKOANI GEITA WAIOMBA SERIKALI KUHAKIKISHA INAKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO)


Ikiwa leo  ni  siku ya kukumbuka watu wenye uaribino  duniani,wananchi mkoani Geita wameiomba serikali kuhakikisha inaweka mipango madhubuti  katika kutokomeza mauaji yanayohusisha watu wenye ualibinism  nhini

Storm habari imezungumza na baadhi ya wananchi  ambapo  wamesema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi  ya watu kuwaua  kwa madai ya kupata mali jambo ambalo halina ukweli wowote na kwamba serikali  inatakiwa kuweka mikakati madhubuti ili kuthibiti suala hilo kwa kutoa elimu kwa wananchi  itakayosaidia kukomesha vitendo hivyo.

Hata hivyo storm habari imezungumza na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo,ambapo amesema kuwa jeshi la polisi limekuwa likitumia mbinu mbalimbali ili kuthibiti mauaji hayo kwa kuwatumia polisi jamii ambao wapo kuanzia ngazi ya vitongoji, ikiwemo pia viongozi wa dini.

Aidha kamanda ametoa wito kwa wananchi kuachana na imani potofu zinazosababishwa watu kufanya vitendo hivyo huku akiwataka kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pindi wanapokuwa na mashaka na baadhi ya watu wanaodaiwa kujihusishwa na vitendo hivyo.

Siku ya albinism duniani ni siku ambayo inaadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 13 june lengo ikiwa ni kutoa elimu kwa watu wenye albinism na kutoa uelewa zaidi kwa watu hawa.

No comments:

Post a Comment