Monday 20 June 2016

JESHI LA POLISI MKOANI GEITA LAZUIA AMATEMBEZI YA AMANI YA CHAMA CHA ACT WAZALENDO



Jeshi la polisi mkoani Geita limezuia matembezi  ya amani ya yaliyoratibiwa na chama cha ACT wazalendo  yaliyokuwa  yamepangwa na viongozi wa chama hicho ngazi ya mkoa, lengo ikiwa ni  kuunga mkono  harakati zinazofanywa na kiongozi wa chama  hicho Taifa, Mh.Zitto Kabwe.

Jeshi hilo limepiga marufuku huku likiwaandikia barua viongozi wa chama hicho, sababu kubwa zilizotajwa  kuzuia matembezi hayo ni kupisha maandalizi ya mwenge wa uhuru na sababu nyingine ikitajwa kwamba kutakuwa na mwingiliano wa  oparesheni  zinazoendelea mkoani hapa.

Storm habari imezungumza na Katibu wa Chama  hicho mkoani hapa Bwana Ikolongo Emmanuel Otoo,ambapo amesema kuwa wanasikitishwa na taarifa ambayo imetumwa na jeshi hilo huku wakiendelea kukiona chama tawala kikiendelea na mikutano mkoani hapa..

Hata hivyo Storm habari  imeshuhudia gari la kikosi cha kutuliza ghasia cha FFU siku ya jana likirandaranda mtaani kwa masaa kadhaa kuimalisha hali ya ulinzi dhidi ya uwepo wa tarifa hizo ambapo matembezi hayo yalikuwa yamepangwa kuanza majira ya saa tatu asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni yakianzia katika uwanja wa Nyankumbu hadi uwanja wa magereza mjini humo.

Aidha wananchi Mkoani hapa wamekuwa na maoni na mitazamo tofauti juu ya kile ambacho kiliweza kuendelea.


Storm habari imemtafuta Kamishina msaidizi wa polisi mkoa wa geita mponjoli mwabulambo na amesema kuwa maandamano yoyote yale yanahitaji askari na sababu ambazo wamezitoa ni za msingi na ni vyema zikazingatiwa katika suala zima la ulinzi na usalama.

No comments:

Post a Comment