Tuesday 7 June 2016

SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF) LAKUBALI KAMATI YA UCHAGUZI YA YANGA IENDELEE NA UCHAGUZI







Shirikisho la soka Tanzania TFF  leo June 7 2016  kupitia kwa Rais wa shirikisho hilo Jamal Malinzi alikaa kikao pamoja na makamu mwenyekiti wa Yanga anayemaliza muda wake Clement Sanga, pamoja na katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit kujadili juu ya makubaliano ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.


Baada ya majadiliano hayo, Rais wa TFF Jamal Malinzi amekubali kamati ya uchaguzi yaYanga kuendelea na uchaguzi wao kama kawaida, ila kamati ya uchaguzi ya TFFitakuwepo tu kwa uangalizi wa uchaguzi huo utakaofanyika June 11 2016.


Maamuzi hayo yanaafikiwa ikiwa ni siku chache zimepita toka uongozi wa Yanga, utangaze kuandaa uchaguzi wao, wakati ambao kamati ya uchaguzi ya TFF ilikuwa imeandaa uchaguzi wa Yanga na wao walikuwa wafanye uchaguzi huo June 25 ila kwa sasa baada ya kuafikiana uchaguzi wa Yanga utafanyika June 11 kama walivyokuwa wamepanga.

No comments:

Post a Comment