Friday 3 June 2016

WANANCHI MKOANI GEITA WALALAMIKIA KUPANDA KWA GHARAMA YA MAZAO YA VYAKULA WAKATI WA MFUNGO WA RAMADHANI

Kupanda kwa bei ya mazao ya vyakula ikiwemo  karanga, viazi, na mihogo, katika kipindi cha mwezi mtukufu  wa ramadhani imeonekana kuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi mkoani geita hususani wenye vipato  vya  chini.

Baadhi  ya  wananchi waishio mkoani   Geita  walipokuwa wakizungumza na Storm habari kwa nyakati tofauti wamesema kumekuwepo na  desturi  ya baadhi ya wafanyabiashara kupandisha  bei   ya vyakula  hivyo  wakati  wa mfungo  wa  ramadhani.

Hata  hivyo  wananchi hao wameiomba  serikali kuhakikisha  kuwa  inaingilia kati jambo hilo  ikiwa ni pamoja   na   kudhibiti ongezeko  la bei  katika kipindi hiki.

 Afisa biashara wa halmashauri ya mji bw, George Mpogomi amesema  kuwa  wananchi walio   na  bidhaa zinazohitajika  kwa kipindi   hiki    ni   vyema wakaanza  kuzipeleka katika  masoko   ili kuondoa upungufu wa bidhaa sokoni jambo ambalo husababisha kupanda kwa  gharama  za mazao hayo.

Aidha Mpogomi  amewashauri wakulima kutumia fursa hiyo kuuza baadhi ya mazao ambayo   yatawasaidia kunyanyua  vipato  vyao.


No comments:

Post a Comment