Friday 10 June 2016

SERIKALI KUTENGA MAENEO KWA AJILI YA WACHIMBAJI WADOGO MKOANI GEITA


Serikali imetangaza kuwatengea maeneo ya kuchimba wachimbaji wadogo wa dhahabu waliopo karibu na mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine (GGM) uliopo mkoani hapa kwa ajili ya kuendelea na shughuli zao za uchimbaji ili waweze kujipatia vipato.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na naibu waziri wa nishati na madini mh Medard Kalemani alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalumu wa jimbo la Geita mjini bi Vick Kamata lililokuwa likiuliza kuwa ni lini serikali itatenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo wanaojishughulisha na shughuli za uchimbaji mkoani Geita.

Kalemani ametaja maeneo hayo ni Mgusu, Nyakabale, Nyamalembo ambapo maeneo ya  Kasubuya serikali imetenga hekta 432,  Matabe hekta 568, Chato hekta 1258  na 232 hekata Geita.


Akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya swali la mbunge wa jimbo la Geita mjini mh Cotantine Kanyasu lililoulizwa kwa niaba yake na mbunge wa viti maalumu bi Vick Kamata lililouliza kuhusu wananchi  kunyang’anya maeneo yao na kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) ambapo amesema kuwa kampuni hiyo ilifanya mazungumzo na wananchi na kuweka makubaliano ya kuwalipa fidia wale wote walioko katika maeneo ya kando kando na mgodi huo na kwamba baadhi yao wamekwisha lipwa fidia zao.

No comments:

Post a Comment