Thursday 2 June 2016

PICHA:MAMA JANET MAGUFULI AMSHUKURU MTUMISHI WA MUNGU TB JOSHUA KWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZAKE ZA KUSAIDIA WAZEE



Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Chama na Wazee wakati akiwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi pamoja na Vifaa vya Malazi.
















Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi, Madawa pamoja na Vifaa vya Malazi.














Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akimueleza jambo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla ya utoaji misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Nkaseka Mkoani Mtwara.



Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara Bw. Rashidi Kambona akimkabidhi taarifa ya kituo hicho Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akiongea na wazee na baadhi ya watu waliojitokeza katika hafla ya utoaji Misaada katika kituo cha kulea Wazee cha Nkaseka Wilayani Masasi Mkoani Mtwara na kumshukuru Mama Janeth Magufuli kwa misaada hiyo na kumuahidi kusimamia ugawaji wa vitu hivyo ili kuepuka kuchukuliwa na watu wasiowaaminifu.



Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na wazee katika kituo cha Nkaseka Mkoani Mtwara na kumshukuru Mtumishi wa Mungu TB Joshua kuunga mkono juhudi zake za kuwasaidia wazee na watu wasiojiweza kwa kuchangia baadhi ya vitu vilivyotolewa kama msaada kwenye kituo hicho.



Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wazee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka kilichopo Mkoani Mtwara.


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (Kushoto) na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa wakimsalimia Moja ya Mzee katika Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka kilichopo Mkoani Mtwara.















 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akifurahia jambo na baadhi ya watoto waliojitokeza katika hafla ya utoaji msaada katika Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka kilichopo Mkoani Mtwara.

No comments:

Post a Comment