Sunday 22 May 2016

FAHAMU FAIDA ZA KULA TUNDA LA PAPAI KIAFAYA

PAPAI IMAGE 1
Asili ya mpapai ni Amerika ya Kati, ambapo kuanzia matunda, majani na utomvu wa mmea huu hutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali duniani. Vile vile, matunda na utomvu wake yamekuwa yakitumika kutengeneza pombe na mvinyo katika baadhi ya nchi, huku wengine wakitumia mpapai kama dawa kwa mifugo na binadamu.
Inaelezwa kuwapo na tafiti zilizowahi kufanyika na kuchapishwa katika jarida lijulikanalo kwa jina la ‘Archieve’ la nchini India mnamo Oktoba 27 mwaka 2010, ambapo jarida hilo lilieleza kwamba juisi ya majani ya mpapai iliweza kusaidia wagonjwa watano waliowahi kupata homa ya dengue.
Mbali na utafiti huo, pia kuna tafiti zilizowahi kufanywa na madaktari wa nchini Marekani na Japani na kubaini kuwa, juisi ya majani ya mpapai ina uwezo wa kutibu malaria na saratani, japokuwa tafiti hizo hazikukubawaliwa kisayansi.
Faida za kiafya za tunda la papai
Tunda la papai lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa
1.Kutibu tatizo la Shida ya kusaga chakula tumboni
2.Kutibu Udhaifu wa tumbo
3.Kutibu Kisukari na asthma au pumu.
4.Kutibu Kikohozi kitokacho mapafuni
5.Kutibu Kifua kikuu

Vile vile Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku
Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda
Vilevile yanasaidia kutibu sehemu palipoungua moto
Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na Ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani)

Pia yanasaidia kutofunga choo
Maganda ya tunda la papai yanasaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.
Mbegu zake zinatibu ini zikitafunwa 10 – 12 kwa siku 5.
Majani yake yakaushie ndani, yanatibu pumu. Inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize, kule kubanwa kutakisha.

Majani yake yanasaidia katika kutibu shinikizo la damu.
Papai likimenywa na kupondwa linafaa Sana katika masuala ya urembo kwani linaweza kutumika Kama vile unavyotumia lotion kulainisha uso.

Mbegu za papai zina uwezo wa kutibu homa. Meza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara 3 kwa ajili ya kutibu homa.

Mbegu za papai zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji, kunywa mara 3 kwa siku 5 Mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda mrefu atapona bila dawa nyingine.

Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita 2 na nusu kwa dakika 15, yanatibu figo, bladder, yanazuia kutapika. Nusu kikombe cha chai kutwa mara 3 kwa siku 5.

No comments:

Post a Comment