Wednesday 15 June 2016

SIKU YA MTOTO AFRIKA KUZIMISHWA KESHO


Tanzania huungana na nchi nyingine za kiafrika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kila mwaka ifikapo june 16, lengo ikiwa ni kukumbuka mauaji ya watoto waliouwawa kinyama na serikali ya makaburu na kusisitiza wajibu wa serikali za Afrika kwa watoto ili kuendeleza haki na maslahi ya watoto nchini.

Mnamo mwaka 1990, uliokuwa umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) ulipitisha azimio la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto kilichopo Afrika ya kusini waliouawa kinyama na iliyokuwa serikali ya makaburu ya nchi hiyo tarehe 16 juni, 1976 ambapo watoto hao walikuwa wakidai haki ya kutobaguliwa na haki nyingine za kibinadamu.

Storm habari imezungumza na wananchi mkoani Geita katika kuelekea siku ya maadhimisho hayo ambapo wamesema kuwa sababu ambazo zimekuwa zikisababishwa kutokea kwa vitendo vya ukatili kwa watoto ni pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya kwa baadhi ya raia na kwamba serikali inapaswa kuhakikisha inachukua hatua kali kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo jambo ambalo litasaidia kutokomeza ukatili nchini.


Maadhimisho haya huambatana na shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo hufanyika kitaifa na kimkoa na kwa mkoa wa Geita yatafanyika kesho katika kijiji cha Lwamgasa kilichopo wilayani na mkoani hapa huku kauli mbiu ya mwaka huu ikisema kuwa “ulawiti na ubakaji kwa watoto vinaepukika chukua hatua”.

No comments:

Post a Comment