Tuesday 7 June 2016

KESI YA ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI KUPITIA FACEBOOK KUSIKILIZWA KESHO JUNE 08 2016









Kesi inayomkabili Isaac Abakuk ambaye anatuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kwenye ukurasa wake wa facebook April 15 2016 imeshindwa kuendelea kutokana na upande wa Jamhuri kutokamilisha ushahidi na kuiomba Mahakama kuahirisha shauri hilo hadi kesho June 08 2016.
 Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Augustine Rwezire wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha amekubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo ambapo inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo, mshtakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana kusubiri kesi yake itakapotajwa.

Mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 17 mwaka huu kinyume na sheria ya mitandao namba 16 kifungu namba 14 ya mwaka 2014 kwa kusambaza ujumbe wa uongo katika mitandao ya kijamii wenye lengo la kumdharau, kumdhihaki na kumtolea maneno Rais Magufuli yenye lengo la kumdhalilisha.
Ujumbe huo ulisomeka, ”Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi bwana.’’ 


No comments:

Post a Comment