Tuesday 7 June 2016

BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU YAKANUSHA UONGO UNAOENEZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII




Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, mwongozo wa utoaji mikopo utatolewa rasmi na kutangazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na tovuti ya Bodi ya Mikopowww.heslb.go.tz

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016

Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz)

No comments:

Post a Comment