Watu kumi na nne (14) mmoja akiwa ni
Raia wa China wamefukiwa na udongo usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba usiku wakiwa wanaendelea na
majukumu yao ya uchimbaji kwenye kampuni ya RZ iliyopo kijiji cha Nyarugusu wilayani na mkoa
wa Geita.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita imefika
katika Mgodi wa RZ kuangalia zoezi
la ukoaji katika mgodi
na kamisha msaidizi wa madini kanda ya
ziwa victoria Mhandisi Yahaya Samamba
ameelezea hali ilivyo na jitihada za uokoaji zinavyoendelea .
Kamanda wa Jeshi
la zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita, Elisha
Mugisha amesema kuwa eneo la chini
ambalo limefukiwa na udongo ndio
ambalo kwa sasa wanaendelea
kulitanua ili sehemu hiyo iwe kubwa
watu waweze kupita.
Mwanasheria na msemajiwa Kampuni ya uchimbaji
Dhahabu ya RZ Fransis Kiganga anaelezea sababu za Mgodi huo kuporomokewa na udongo.
Baadhi ya
wafanyakazi wa Kampuni hiyo Charles Julius na Robert Stanley ambao ni wachimbaji wa kampuni hiyo wanaelezea hali ilivyokuwa
na namna ilivyotokea.
Aidha mkuu
wa mkoa wa Geita Meja Jenerali mstaafu ezekiel kyunga amewataka
wanaosimamia zoezi la uokoaji kuongeza
nguvu ya uokozi.
No comments:
Post a Comment