Baadhi ya
wafanyakazi wakizungumzia hali ilivyokuwa juu ya kuwepo kwa taarifa ya kupigwa
kwa wenzao mgodini hapo.
Sakata la watu wawili wanaodaiwa kupigwa na raia wa kigeni wa China
akiwemo aliyelazwa katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Geita limechukua
sura mpya baada ya kubainika chanzo chao cha kupigwa ni kuiba mawe
yanayodhaniwia kuwa na dhahabu na maji walipokuwa wakifanya kazi katika
mgodi wa wa dhahabu unaomilkiwa na kampuni ya RZ uliopo katika kijiji cha
Mawemeru wilaya na mkoani Geita na siyo kutokana na madai kupandishwa
mishahara.
Tukio hilo limetokea Januari 19 wakati wa zamu ya usiku baada ya
mfanyakazi Benedict Lumimi Maduhu kudaiwa kukamatwa akiwa na mawe
yanayodhania kuwa na dhahabu ndani ya mgodi huo wakati akiwa zamu usiku
na baada ya kukamatwa rafiki yake wa karibu na ndipo rafiki yake wa
Karibu Elisha Silivester [26] ambaye naye anatuhumiwa kwa kuiba maji
alifanikiwa kukimbia hadi kituo cha polisi cha Nyarugusu kutoa taarifa
kuwa yeye na mwenzake walikuwa wakipigwa na wachina baada ya kudai
waongezewe mshahara.
Akithibitsha tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli
Mwabulambo amesema wafanyakazi Bedeicto Lumimi Maduhu walikamatwa na polisi
kutoka ndani ya mgodi huo baada ya kukuta tayari amekamatwa na kufungwa
kamba na wafanyakazi wengine wa mgodi huo tayari kwa kumpeleka kituo cha polisi
cha Nyarugusu pamoja na mawe yanayodaiwa kuwa na dhahabu .
Ameongeza kuwa Elisha Silvesta anayedaiwa kuiba maji yeye ndiye
aliyekimbia na kutoa taarifa kituo cha polisi baada ya kufanikiwa kutoroka
kabla ya kukamatwa na polisi baada ya kufika eneo la tukio waliwachukuwa
watuhumiwa Benedicto pia wafanyakazia baadhi wa mgodi huo hadi kituo cha
polisi kwa mahojinao ikiwani pamoja na kuwahoji baadhi ya wafanyakazi wa
mgodi huo akiwemo Elisha mwenywe.
''Taarifa rasmi za uchuguzi ni kuwa chanzo cha kupigwa kwao ni
kutuhumiwa kwa wizi wa mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu na
maji kama nilivyoeleza sisi kama polisi pia baada ya kutokea malalamiko hayo
kutoka kwa watuhumiwa pia wanaotuhumiwa tulichukua jukumu la kuwakamata
na kuwahoji na kinachoendelea sasa ni mchakato wa kukusanya
ushahidi kwa hatua za kisheria hivyo chanzo ni cha wao kupigwa ni
kutuhumiwa na siyo madai ya nyongeza za mshahara”alidai Mponjoli.
Hata hivyo polisi imebainisha wazi kuwa zipo changamoto kwa baadhi ya
watu kujenga hoja zinazolenga kujipatia
fedha kutoka kwa wachina kwa kujenga hoja ya kupigwa na kujeruhiwa
vitendo alivyodai polisi haina budi kuyafanyia kazi kwa umakini madai
hayo kwa vile tayari ipo mifano ya matukio ambayo yaliwasilishwa lakini
yakaisha kwa walalamikaji kudai pesa na kutelekeza kesi zao.
Ametoa mfano tukio lililtokea julai 6 mwaka jana la Masanja
Shilomero[25] mkazi wa kijiji Nyamitondo kudai kushambuliwa na wajiri
wake ambao ni raia wa china na kufunguliwa kesi namba CC/278/2016 mlalamikaji
aliitelekeza kesi hiyo baada ya kudaiwa alikuwa ameomba na kupewa fedha kutoka
kwa walalamikiwa na kuitelekeza kesi yake.
Kesi hiyo kushindwa kuendelea na siyo kwamba imetelekezwa na
polisi,na tukio jingine amelitaja kuwa ni mchimbaji Richard Kasubi
anayelalamikiwa na baadhi ya watu wanaodaiwa kufanya kwake kazi ya kushusha
mifuko ya saruji kutoka katika gari kuiweka katika
ghala lake badaye walidai kudhurika hata hivyo tayari
inadaiwa walilipwa pesa na mlalamikiwa huyo baada ya kutaka malipo kwa ajili ya
matibabu na baada ya kiasi cha shilingi 500,000 wanachodaiwa kupewa kukimaliza
walianza tena kudai upya na hivyo kuibua mgogoro.
kutokana na uwepo wa mazingira ya aina hiyo polisi wanatakiwa kufanya
kazi kwa umakini ili kutenda haki kwa pande zote na kuwa Benedicto na wenzake
tayari amefunguliwa kesi ya wizi wa mawe yanaodhaniwa kuwa na dhahabu
katika kituo cha polisi cha Nyarugusu na upelelezi wake unaendelea ikiwemo
wanaodaiwa kuwapiga nao wamefunguliwa kesi na inachunguzwa.
Awali akizungumzia matukio hayo Meneja wa mgodi huo wa RZ Gui Xue Liu
kupitia msemaji wa kampuni hiyo Francis Beatus Kiganga amesema vitendo vya wizi
kwa wafanyakazi wanavyofanya na kisha kuwageuzia kibao kunaweza kuwakatisha
tama kuwekekeza katika sekta hiyo ya madini kwani imekuwa ikiwapa
usumbufu mkubwa.
Amesema kwa kawaida wao wamekuwa wanapowakamata watuhumiwa huamua
kuwafukuza kazi badala ya kuwapeleka
kwenye vyombo vya sheria ili kuepuka kupoteza muda na usumbufu na
watuhumiwa kutumia mwanya huo huwageuzia kibao hatua waliyodai inaonekana
kuwaathiri na kuiomba serikali kulifanyia kazi kwa umakini wimbi hilo la
wachina kutuhumwia kupiga watumishi.
Mganga wa zamu katika hospitali hiyo Elias Hambuhambu amethibitisha juzi
jioni kwa Elisha Sivesta kulazwa hospitalini hapo kwa madai ya kupigwa na kuwa
hata hivyo hali yake ilikuwa inaendelea vizuri na alikanusha uwepo
uvumi wa kujeruhiwa sehemu za siri za majeruhi huyo kwani alikuwa
amewekewa mpira wa haja ndogo kama hatua ya kawaida kwa wagonjwa
wanaolazwa wanaokuwa na madai ya kusikia maumivu ya mwili.
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo wakiwemo Amani Silivesta na Annicent
Masanja walidai mwenzao elisha aliondoka kwenda kuropiti Kituo cha polisi
akijihami baada ya Benedicto kukamatwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa na
dhahabu wakati alipokuwa zamu ya usiku na waliondoka na Polisi baada ya
yeye kwenda kutoa taarifa na wakati huo wote hakuwa amepigwa na madai ya
kupigwa yamejitokeza siku mbili baada ya kutokea uhalifu huo hivyo kuibua sintofahamu.
Akizungumzia tuhuma hizo Elisha Silvesta akiwa wodini alimolazwa juzi
katika hopitali teule ya mkoa wa Geita alikiri kuwa chanzo cha wao yeye na
Benedicto kupigwa ni kutuhumiwa yeye kuiba maji na mwenzake Benedicto
kuiba mawe yanaodhaniwa kuwa na dhahabu na baada ya kufanikiwa
kukimbia alikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi Nyarugusu kuwa
mwenzake Benecto Lumimi Maduhu alikuwa amefungwa kamba akipigwa bakora na
wachina ili kujihami.
No comments:
Post a Comment