Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akikagua gwaride katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika
katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Vijana
vya halaiki wakiwa katika umbo linaloonesha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akiongea na wananchi wakati wa sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar ambapo alisema mbali na jitihada zilizofanywa na serikali hiyo katika
kuinua maisha ya Wazanzibar ameahidi kuendelea kusimamia rasilimali ili
zitumike kwa maslahi ya wananchi wote.
Zanzibar imeadhimisha
miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu huku ikiwa imepiga hatua mbalimbali za
kimaendeleo na utoaji wa huduma bora za kijamii.
Hayo yamebainishwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya Mapinduzi leo
katika uwanja wa Amani, Unguja, Zanzibar.
Dkt. Sein amesema kuwa
siku ya Mapinduzi ni muhimu sana katika historia ya Zanzibar kwani ndiyo siku
ambayo Wazanzibar walipokuwa huru katika nchi yao na kuweza kufanya shughuli
mbalimbali za kujiletea maaendeleo.
“Tukiwa tunasherehekea
miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni vyema tukajivunia maendeleo
yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana.”Alisema Dkt. Shein.
Akitaja baadhi ya
mafanikio yaliyopatikana tangu Mapinduzi Matukufu yatokee tarehe 12 Januari
1961, Dkt. Shein amesema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta za elimu
kwa kuwa na ongezeko la shule kutoka shule 752 mwaka 2015 hadi kufikia 843
mwaka 2016.
Ongezeko hilo limeenda
sambamba na ongezeko la udahili wa wananfunzi ambapo umeongezeka kutoka
wanafunzi 384,000 hadi kufikia 424,000 mwaka 2016.
Katika sekta ya afya
kumekuwa na mafanikio ya kuongezeka kwa vituo vya afya kwa asilimia 13.4 ambapo
mwaka 2015 kulikuwa na Vituo vya Afya 134 hadi kufikia sasa jumla ya Vituo 152
vimepatikana.
Mafanikio mengine ni
pamoja na upatikanaji wa ajira 2658 zilizotokana na miradi mbalimbali
iliyozindulia katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku ya Mapinduzi, kukua
kwa Sekta ya Utalii kwa ongezeko la watalii kwa asilimia 13 huku ikichangia
pato la taifa kwa asilimia 27.
Huduma za kijamii
zimezidi kuboreshwa huku upatikanaji wa maji safi na salama umeendelea
kutatuliwa ambapo miradi ya maji imeekuwa ikitekelezwa ikiwemo kuchimba visima
vipya 9 na kuvifanyia ukarabati visima vya zamani.
Kwa upande wake Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema
kuwa Mapinduzi haya yamekuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa kuwa yamewaweka
Wazanzibar kuwa huru katika kutekeleza shughuli zao za kujiletea maendeleo.
Zanzibar imeadhimisha
miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar huku ikiwa imepiga hatua kubwa za
kimaendeleo ambapo katika shamra shamra za maadhimisho haya jumla ya miradi 32
ya maendeleo imezinduliwa huku mingine 16 ikiwekwa jiwe la msingi tayari kwa
utekelezaji wake, hayo yote ni matunda yatokanayo na Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar ambayo baadaye yalizaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment