Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya kupiga kura kutoka kwa msimamizi
Askari polisi wakiimarisha ulinzi katika kituo cha kupigia kura
Kata ya Nkome wilaya na Mkoa wa Geita, imefanya
uchaguzi mdogo wa udiwani huku hali ya ulinzi na usalama ikitawala katika
kipindi chote cha upigaji wa kura.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Geita Ali Kidwaka ameelezea kuwa zoezi hilo limefanyika katika
hali ya utulivu na kwamba jumla ya vituo thelathini na nane (38) vimehusika
kufanya uchaguzi.
Kuhusu ulinzi
na usalama Kidwaka amesema kuwa hali ilikuwa tulivu hakuna fujo wala usumbufu
wowote ambao umeweza kujitokeza lakini nje ya vituo kuna masuala yalijitokeza
ya uvunjifu wa amani na utulivu.
Baadhi ya wananchi wa kata hiyo Hussein Omary
ameeleza kuwa uchaguzi ambao umefanyika katika hali nzuri kwani hayupo ambaye
ameshindwa kupiga kura vituo vyote vilikuwa wazi na kwamba kila mtu alikuwa ana
uhuru wa kumchagua yule ambaye anaona yupo sahihi kumwongoza.
Naye Bi.Flora Mussa amesema kuwa wao kama wazee
wanaishukuru serikali kwani hakuna buguza ambayo wamekutana nayo na kwamba
wamekuwa wakipewa nafasi ya upendeleo na kuthaminiwa katika chumba cha
uchaguzi.
No comments:
Post a Comment