Tuesday, 10 January 2017

MTI WAZUA KIZAZAA MKOANI GEITA



Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wa mtaa wa samina kata ya mtakuja wilaya na Mkoa wa Geita  wamejikuta wakiingiwa na taaruki ni baada ya mti  mbwa ulionguka kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kukuta  umesimama  wenyewe.
Baadhi ya wananchi katika Mkoa wa Geita na Viunga vyake wamechimba mizizi ya mti huo pamoja na kuchukua magome yake kwa madai ya kwenda kuomba matatizo yao.

 wananchi  waliokuwepo kwenye eneo la tukio walisema kuwa mti huo ulianguka tangu mwaka 2011 na jana majira ya saa sita mchana walipata habari kuwa mti huo umesimama

Mwenyekiti wa mtaa huo John Barenge pamoja na mzawa mmoja Abudara wamesema sehemu hiyo wazee wa zamani walikuwa wanaitumia kwa ajili ya matambiko kwa kutibu watu.

Diwani wa kata  ya mtakuja Constatine Molandi amewataka wananchi wake kutotumia mizizi na magome ya  mti huo kwa ajili ya kunywa kwani hakuna anayejua madhara ambayo yanaweza kujitokeza .


Baadhi ya wazee ambao awakutaka kuchukuliwa sauti zao  wala kuandikwa majina yao wamesema kuwa mambo haya yanaanza kutokea kwa sababu imeandikwa kwenye vitabu vya mungu.

No comments:

Post a Comment