Rais wa Jmamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameuagiza uongozi wa Mkoa
wa Shinyanga kumfutia usajili mwekezaji wa Kiwanda cha Nyama, Kampuni ya Triple
S na badala yake watafute mwekezaji mwingine.
Agizo hilo limetolewa
leo Mjini Shinyanga wakati akiwahutubia wananchi wa mji wa huo ambapo yupo
mkoani humo kwa ziara ya kikazi iliyoambatana na sherehe ya kuadhimisha miaka
53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
“Futeni usajili wa
mradi wa Triple S, haiwezekani mwekezaji hakashindwa kuendesha kiwanda kwa
zaidi ya miaka 10 sasa afu tuendelee kumkumbatia, tafuteni mwekezaji mwingine,
mkishindwa semeni Serikali iweke hela, ili uzalishaji uendelee,” alisisitiza
Rais Magufuli.
Aliongeza kuwa
mwekezaji huyo amekuwa mbabaishaji kwani tangu kipindi yeye (Rais Magufuli)
alipokuwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo alimfahamu na alimpa maelekezo cha
kusikitisha hakuna jambo aliloendeleza ikiwemo kuanza kwa uzalishaji.
Akizungumzia sababu ya
kufanya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar katika upande huu wa Bara Rais
Magufuli amesema kuwa Tanzania ni moja, na kuongeza kuwa chimbuko halisi la
uwepo wa Taifa la Tanzania ni Mapinduzi ya Zanzibara mabapo miezi michache tu
baada ya kufanyika kwa mapinduzi hayo Tanganyika na Zanzibar ziliungana na
kuzaliwa kwa Taifa la Tanzania.
Kwa upande wake Waziri
wa TAMISEMI na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari
Heri amesema wao kama Wazanzibar wamefarijika sana kwa kitendo cha Serikali ya
Awamu ya Tano kuamua kushiriki maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu kwa
kusherehekea katika upande wa Bara kitu ambacho akijawahi kufanyika kabla.
Aliongeza kuwa ujio
wake umetokana na ukweli kwamba Tanzania ni nchi moja hivyo Rais Magufuli
alivyoeleza nia yake ya kuadhimisha Maapinduzi huku Bara, Rais Dkt. Shein
alimteua aje kumwakilisha na kueleza kuwa maefarijika sana na kusema Tanzania
ni yetu sote na tutaendelea kuwa wamoja.
Rais Dkt. Magufuli
yuko ziarani Mkoani Shinyanga ambapo kesho anatarajiwa kufungua viwanda kadhaa
vilivyopo mkoani hapo, baadhi ya viwanda hivyo ni pamoja na Kiwanda cha
Vinywaji Baridi (maji) cha Jambo, Kiwanda cha Mafuta na vingene.
No comments:
Post a Comment