Mwenyekiti
wa Kitengo cha Nafaka na Mamalishe wa Soko la Kisutu jijini Dar es
Salaam,Bw. Mohamed Salum akielezea jambo
kwa mwandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula katika Soko hilo
leo jijini Dar es Salaam. Mohamed amesema kuwa chakula kinapatikana kwa wingi
kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa.
Picha
ikionyesha baadhi ya nafaka zikiwa zinauzwa katika Soko la Kisutu jijini Dar es
Salaam.
Mkazi
wa jijini Dar es Salaam akinunua nafaka katika Soko la Kisutu jijini Dar es
Salaam
Hali ya upatikanaji wa chakula nchini inaridhisha
licha ya changamoto ya kuongezeka kwa bei ya bidhaa za chakula zitokanazo na
nafaka.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kitengo cha
Nafaka na Mamalishe wa Soko la Kisutu jijini Dar es Salaam, Bwana Mohamed Salum
katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam.
Mohamed amesema kuwa pamoja na kuwa Dar es Salaam
inategemea chakula kutoka mikoani bado hali ya upatikanaji wake ni mkubwa na wa
kuridhisha kama ambavyo imekuwa miaka ya nyuma.
“Chakula bado kinapatika kwa wingi japo changamoto
iliyopo ni ongezeko la bei pekee kitu ambacho si kigeni duniani kote,” alisema
Salum.
Alisema nia ajabu sana kusikia watu wanasema kuna
baa la njaa wakati vyakula vinapatikana kwa wingi katika masoko yetu.
Aliongeza kuwa kungekuwa na tatizo la uhaba wa
chakula basi hata uingizwaji wa chakula katika jiji la Dar es Salaam ungepungua
kwani asilimia kubwa inategemea chakula kutoka mikoani, badala yake upatikanaji
wa chakula umeendelea kuwa wa kuridhisha.
“Ndugu mwandishi ukitaka kujua kuwa hakuna uhaba wa
chakula jaribu kutembelea maeneo ya Manzese Uzuri utajionea namna maroli matani
kwa matani yanayoingiza nafaka kwenye mashine za kusaga na kukoboa.”
Alisisitiza.
No comments:
Post a Comment