Baadhi ya wananchi wa kata ya Katoro wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya
Geita ,Mwl Herman Kapufi wakati alipokuwa akizungumzia swala la ushiriki wa
wananchi katika uchangiaji wa maendeleo katika kata hiyo
Baadhi ya wananchi wakifatilia kwa makini kilichokuwa kikizungumzwa katika mkutano
Wananchi wa mamlaka ya mji Mdogo wa Katoro Mkoani Geita, wamekubali
utendaji wa kazi alioanza nao Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Heriman Kapufi wa
kuzunguka na kuzungumza na wananchi kusikiliza kero zao na kuzitatua
swala ambalo ni kinyume na viongozi baadhi ambao wamepita hapo nyuma.
Wakizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji
wa Katoro wananchi hao walisema kuwa Mkuu huyo wa wilaya ameletwa na mwenyezi
Mungu hivyo wanaimani naye kuwa atakuwa mstari wa mbele kutatua kero
zinazowakabili.
Katika Mkutano huo wananchi walitoa changamoto mbalimbali, huku sekta ya
afya ikilalamikiwa na wananchi wengi ambapo akina mama walisema wamekuwa
hawapatiwi huduma inayotakiwa.
“Mkuu wetu wa wilaya tukueleze tu, sisi hatuna mashaka na wewe kwa jinsi
ulivyo umekuwa na hofu ya Mungu tunajua maendeleo kwa wilaya yako ya Geita
yatakwenda kwa kasi viongozi wengi hapa Geita wamekuwa wakitusimamia na
kututofautisha kutokana na hali zetu za kimaisha mambo yaliyokuwa
yakikwamisha kutokana na migongano watu wa Katoro tulikuwa wachangiaji
wakubwa katika maendeleo ya kata yetu,’’ alisema mkazi wa katoro
DC Kapufi ambaye amekuwa akimtanguliza Mungu katika vikao vyake na
mikutano mbalimbali ya wananchi, huku akiuhubiri upendo kwa wananchi
jambo ambalo limewavutia wengi huku wakiahidi kumpa ushirikiano ili kuijenga
Katoro na Geita kwa ujumla ambayo imetawaliwa na itikadi za kisiasa huku
miradi mbalimbali ya maendeleo ikikwamishwa na baadhi ya wanasiasa.
No comments:
Post a Comment