Kaimu
Mkuu wa Kitengo Cha Habari toka Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA) Mhandisi Yisambi Shiwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini
Dar es salaam kuhusu mafanikio ya wakala huo katika kipindi cha Julai-Desemba
2016 ikiwemo kufanikiwa kukusanya Bilioni 79.26 zilizolipwa Serikalini na
Kampuni za Madini kama kodi ya mapato. Kushoto ni Meneja Utafiti na Mipango wa Wakala huo Bw. Julius Moshi na
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya Madini Migodi Mikubwa, ya
Kati na Midogo Mhandisi Baraka Manyama.
Meneja
Utafiti na Mipango wa Wakala wa Ukaguzi wa
Madini Tanzania (TMAA) Bw. Julius Moshi akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa
na wakala huo katika kuhakikisha kuwa Serikali inakusanya mapato yote yanayotokana
na Madini.
Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya wakala huo kusimamia
vyema sekta ya madini ili iweze kulinufaisha Taifa. Kulia ni Meneja Utafiti na
MipangowaWakala waUkaguzi waMadini Tanzania (TMAA) Bw. Julius Moshi.
Baadhi
ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA) leo Jijini Dar es salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya
madini migodi mikubwa,ya kati na midogo Mhandisi Baraka Manyama akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu kupatikana kwa malipo ya mrabaha kutokana
na shughuli za uchenjuaji wa marudio kwa kutumia teknolojia ya VAT LEACHING. Kulia
ni Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza na kushoto ni Meneja Utafiti na Mipango Bw. Julius Moshi.
Kaimu Mkurugenzi wa ukaguzi wa hesabu za Kodi na fedha za Migodi Bw. Venance Bahati akieleza
kwa waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya wakala huo kukagua migodi yote na
kuhakikisha kuwa Kodi zote zinalipwa Serikalini kwa kuzingatia sheria na kanuni
zinazosimamia sekta ya madini , kulia ni Meneja wa uthamini
wa Madini Bw.George Kaseza na kushoto ni
Meneja Utafiti na Mipango Bw. Julius Moshi.
No comments:
Post a Comment