Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa muda kwa waraka uliotoa muungozo wa matumizi ya Mihuri kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza na baadhi
ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji jijini Dar es Salaam kuhusu uamuzi wa
Serikali wakusitisha kwa muda katazo la Wenyeviti hao kutumia Mihuri ya Ofisi na
badala yake utaratibu wa awali uendelee hadi hapo hatua nyingine zitakapochukuliwa.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Boniphace Simbachawene akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Mkoa
wa Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu
uamuzi wa Serikali wa kusitisha kwa muda katazo la Wenyeviti hao kutumia Mihuri
ya Ofisi na badala yake utaratibu wa awali uendelee kutumika hadi hapo hatua nyingine
zitakapochukuliwa.
Serikali imesitisha
waraka wa muongozo uliotolewa kuhusu matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa Mitaa
na vijiji mpaka pale itakaposhirikiana na kukubaliana namna bora ya kuendesha
masuala ya kuhudumia wananchi.
Akizungumza na baadhi
ya wenyeviti wa mtaa, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amewataka wenyeviti wa mitaa nchini
kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.
Mhe.Simbachawene
alisema kuwa nia ya kusitisha waraka huo ni kuweka utendaji mzuri baina ya
Serikali na watendaji wake wa chini.
“Utaratibu uliopo
uendelee mpaka pale Serikali itakapotoa utaratibu mwingine wa matumizi
mbalimbali ya mihuri hiyo baada ya kujadiliwa na kushirikiana vya kutosha”
alifafanua Waziri Simbachawene.
Mhe.Simbachawene
alisema kuwa kuna baadhi ya wenyeviti wa mitaa wamekuwa wakitumia vibaya mihuri
hiyo na kupelekea migongano na migogoro ya ardhi katika vijiji na mitaa ikiwemo
maeneo ya Ununio, Temeke.
Mbali na hayo alisema
kuwa katika Tangazo la Serikali namba 3 lililotolewa 5 Septemba, 1994 limeeleza
baadhi ya vitendea kazi vya mwenyekiti wa mtaa ni bendera yenye nembo ya
Halmashauri, daftari ya kutunza kumbukumbu na rejista ya makazi.
Alisema kuwa mamlaka
ya mwenyekiti haitokani na mihuri, bali utendaji uliopo ndani ya mtaa au kijiji
husika, hivyo mamlaka ya mwenyekiti ipo pale pale na haibemwi na muhuri bali
muhuri huonesha nguvu ya ofisi baada ya kuwashirikisha watendaji tofauti ndani
ya kijiji katika kutoa maamuzi.
“Mhuri si mali
ya mwenyekiti binafsi, hivyo kwa yeyote atakayekiuka matumizi ya mihuri hiyo
Sheria itachukua mkondo wake” alisisitiza Mhe. Simbachawene.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Temeke Bakiri Makele,
ameahidi kushirikiana na Serikali kwa kutumia mihuri hiyo kwa kufuata Sheria na
taraibu zilizopo.
Naye Katibu wa
Wenyeviti hao, Marium Machicha alimshukuru Waziri mwenye dhamana kwa kauli
aliyoitoa baada ya kuliona tatizo hilo na kuahidi kulifanyia kazi.
Serikali ilitoa
Muongozo huo wa namna wa matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa mitaa na vijiji
kwa sababu ya matumizi mabaya ya mihuri kwa baadhi ya wenyeviti wa mtaa na
vijiji nchini.
No comments:
Post a Comment