Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi(Kushoto) na Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe(Kulia)
Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi amewaasa wafugaji kuacha kuingiza
mifugo katika hifadhi za taifa ili kuzitunza hifadhi hizo.
Katibu Mkuu uyo aitoa
wito huo wakati akizungumza baada ya kufanya matembezi ya kupinga ujangili
unaofanywa dhidi ya Tembo ya kilometa 5 kutoka Ubalozi wa China mpaka Hoteli
ya Sea Cliff ambapo wageni mashughuli kama Rais Mstaafu wa awamu ya tatu
Mhe.Benjamini William Mkapa alishiriki.
“Hifadhi za taifa hapa
nchini hazina budi kulindwa na kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi
kwani maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya wanyama pori pekee na siyo kwa
mifugo na hivyo kila mwananchi analo jukumu la kuyalinda
mazingira haya,”Aliongeza Mej.Gen Milanzi.
Awali akizungumza katibu
mkuu huyo alisema kuwa Serikali ina mkakati mkubwa wa kuhakikisha inashirikiana
na nchi zingine katika kutokomeza kabisa Ujangili wa pembe za ndovu nchini.
Aidha aliishukuru Serikali
ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na
ujangili wa pembe za ndovu ikiwemo upigaji marufuku biashara ya pembe za ndovu na viwanda
vya kuchonga pembe hizo ifikapo mwezi machi Mwaka huu.
Mbali na hayo katibu
Mkuu uyo amewaasa watanzania kuwafichua wale wote wanaojihusisha na biashara
hiyo na kuonya kuwa kwa kushiriki katika biashara hii tutawafanya tembo wetu
kuwa historia kwani hawatakuwepo tena.
Naye Rais Mstaafu wa awamu ya
tatu Mhe.Benjamini William Mkapa amewataka watanzania kulinda na kutunza mbuga
zetu kwani ni urithi wa kila mtanzania na kuzitaka nchi mbalimbali kusaidia
katika kulinda urithi huu wa wanyama na kuvitaka vyombo vya habari kushiriki
vyema katika kutangaza mbuga zetu na pia kutangaza jitihada zinazofanywa na
serikali katika kutokomeza ujangili wa pembe za ndovu.
No comments:
Post a Comment