Mchungaji wa Kanisa FPCT Geita
Mathias Gundula ,Akimshukuru Mungu juu ya yale ambayo ameyateda kwa
vijana ambao wameokolewa kutoka mgodini.
Mkuu wa
Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiwasalimia wachimbaji
ambao walikuwa wamefukiwa na kifusi kwenye Mgodi wa RZ,katika Hosptali ya Rufaa
ya Geita.
Wahanga 15
wakiwemo watanzania 14 na Raia mmoja wa kichina walionusurika na kifo baada ya kuokolewa kutoka chini ya ardhi
kwenye mgodi wa dhahabu wa RZ Union
ulioko kijiji cha Mawe-meru kata ya Nyarugusu mkoani Geita baada ya kukaa
siku 3 bila chakula wala huduma wameruhusiwa kutoka hospital ya mkoa wa geita
walikopelekwa kupata matibabu.
Akiwaaga baada ya kuruhusiwa
kutoka hospitali mkuu wa mkoa Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amewaomba kurudi na kuendelea kujituma katika
shughuli ambazo wanafanya ili kuendelea
na ujenzi wa taifa.
Hata hivyo mkuu wa
Wilaya ya geita Herman Kapufi,amesema kuwa wamekubaliana na mgodi huo
wafanyakazi wote katika mgodi huo kupatiwa mkataba ambao utawasaidia
wafanyakazi na pia amewaomba kuwa na mahusiano mazuri baina ya wafanyakazi na waajiri
ambo ni raia wa china na pia amewasisitiza kumrudia mungu kwani amewanusuru na
kifo.
Aidha kwa upande
wake mwanasheria wa mgodi huo Francis Kiganga pamoja na kuyashukuru mashirika ambayo
yamejitolea kufanya shughuli za uokoaji
pia amemwakikishia mkuu wa wilaya
kuongeza mkataba wa kazi badala ya miezi mitatu
atawapatia wa mwaka mzima.
Akiwaruhusu wahanga
hao, mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Geita Dkt. Brian Mawalla amesema
wamefikia uamuzi wa kuwaruhusu baada ya kujiridhisha na maendeleo mazuri ya afya
zao.
Wahanga hao
wameokolewa January 29 mwaka huu kwa msaada kutoka makampuni ya Busolwa Mining,
Nyarugusu , Geita Gold Mine(GGM) , na ACACIA Mining wamefanikiwa kuwaokoa watu
hao waliofukiwa na udongo wa kifusi cha mgodi huo januari 26 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment