Uhusiano uliopo kati ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya watu wa china ni kichocheo
kikubwa cha maendeleo baina ya pande zote mbili.
Makamu wa Rais Mhe. Samia amesema kuwa Rais Dkt.
John Pombe Magufuli anatambua umuhimu wa ushirikiano huo na ameipongeza
Serikali ya China kwa kuwa mshirika muhimu katika kusaidia utekelezaji wa
miradi mbalimbali nchini.
Miradi hiyo inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya
watu wa China inajumuisha Sekta za Elimu, Afya, Kilimo Ujenzi na Uchukuzi.
“Ushirikiano uliopo kati ya nchi yetu na China
utawezesha Tanzania kujenga viwanda ambavyo vitasaidia kukuza uchumi wa nchi na
kuongeza pato la taifa,” alisema Mhe. Samia.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania,
Dkt. Lu Youqing amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya dhati ya kuwaletea maendeleo Watanzania
pamoja na kupambana na rushwa.
Dkt. Lu Youqing amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Serikali
ya China itaendelea kushirikiana na Tanzania kama ilivyoasisiwa na waasisi wa
mataifa hayo.
Ni desturi kwa taifa la China kuadhimisha mwaka mpya
na kuupa majina tofauti kulingana na miaka, mwaka huu wa kichina unaitwa ‘mwaka
wa Kuku Jogoo’ ambao hutokea kila baada ya miaka 60.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
Serikali akiwemo Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses
Nnauye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Dkt. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima, Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage, jamii ya wachina waliopo Tanzania.
No comments:
Post a Comment