Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alifika katika kijiji cha Tindiga kilichopo
wilaya ya Mikumi zilipotokea vurugu zilizopelekea mkulima mmoja kuchomwa mkuki
mdomoni na kutokea shingoni na kusikiliza kero zinazowasumbua wananchi wa
Kilosa kabla ya kutoa maamuzi.
Waziri Mwigulu amesema kuanzia sasa likitokea tukio
lolote la watu kuuana kwa mapanga, mikuki, sime na silaha zozote za jadi
zinazotumiwa hasa na wakulima na wafugaji, serikali itafuta utaratibu wa kubeba
silaha hizo na atakayebeba atakamatwa na kuchukuliwa hatua kama watuhumiwa
wengine.
Kinginie alichoagiza Waziri
Mwigulu ni wakuliam na wafugaji kwa pamoja kuwakamata watu wote watakaohusika
na kuanzisha vurugu na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola kabla jeshi la polisi
halijafanya maamuzi yake.
“Kuanzia leo tunaanza kuhesabu
pakitokea tukio lolote la vurugu na zikatumika silaha kuwadhuru wananchi,
tutafuta utaratibu wa watu kutembea na silaha mitaani, na ukikutwa nayo
unakamatwa kama ambavyo mtu mtu mwenye silaha ya moto na hajaiandikisha.
Hatuwezi kuruhusu hii ikawa nchi ya watu wanakatanakatana tu” – alisema Mwigulu
No comments:
Post a Comment