Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (aliesimama)
akifungua mafunzo elekezi juu ya tozo za matengenezo ya magari, pikipiki na
mitambo kwa watumishi wa TEMESA kutoka mikoa 19. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uzalishaji na
Matengenezo Mhandisi Sylvester Semfukwe na kulia ni Meneja wa TEMESA Dodoma. Mafunzo
hayo ya siku 5 yanafanyika Mkoani Dodoma katika ukumbi wa TBA.
Washiriki
wa mafunzo elekezi juu ya tozo za matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yanayofanyika
Mkoani Dodoma katika ukumbi wa TBA wakisikiliza hotuba ya Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (hayupo pichani). Mafunzo
hayo ya siku tano yanashirikisha watumishi wa TEMESA kutoka mikoa 19.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo elekezi juu ya tozo za matengenezo ya magari, pikipiki
na mitambo yanayofanyika mkoani Dodoma katika ukumbi wa TBA wakiwa kwenye picha
ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa
Iddi Mgwatu (alieketi katikati) baada ya ufunguzi. Mafunzo hayo ya siku tano
yanashirikisha watumishi wa TEMESA kutoka mikoa 19.
Mameneja
kutoka mikoa 19 yenye vituo vya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiwa
kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Iddi Mgwatu
(alieketi katikati) baada ya ufunguzi wa mafunzo elekezi juu ya tozo za
matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo yanayoendelea mkoani Dodoma katika
ukumbi wa TBA
Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Iddi Mgwatu amefungua mafunzo elekezi
kwa mameneja wa mikoa na vituo vya TEMESA juu ya tozo za matengenezo ya magari,
pikipiki na mitambo pamoja na uaandaji wa taarifa za uzalishaji za mwezi kwa
watumishi wa TEMESA kutoka katika mikoa na vituo mbali mbali vilivyopo nchini.
Katika hotuba yake Dkt.
Mgwatu amewataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanashiriki mafunzo hayo kwa
umakini mkubwa ili kuleta mabadiliko chanya kwa TEMESA na kuondoa kero
mbalimbali zilizopo sasa, ikiwemo kero ya gharama kubwa za matengenezo ya
magari, pikipiki na mitambo ya serikali na kuwataka watumishi hao kuondokana na
wazabuni wanaouza vipuri na vilainishi vya magari kwa bei ghali isiyo ya soko.
“Mafunzo haya ni
gharama na kwa hiyo haitakuwa jambo jema tukarudi katika vituo vyetu na
kuendeleza mambo yale yale kwa mazoea. Tutakuwa hatujatenda haki kwa wananchi
na kwa taifa kwa ujumla. Niwe mkweli kuwa nitachukua hatua kali pale
nitakapoona mkoa au kituo hakifanyi vyema katika utendaji kazi wake” alisema
Dr. Mgwatu.
Nae Mkurugenzi wa Idara
ya Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Semfukwe amesema kuwa idara
yake imeandaa mada mbali mbali kwa ajili ya mafunzo hayo zikiwemo: Tozo ya
matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo kwa kuzingatia muda halisi wa
matengenezo, Mfumo mpya wa kuandaa taarifa za uzalishaji za kila mwezi, Namna
ya kubaini vipuri bandia kwa njia ya kielektroniki, Masuala ya masoko na huduma
kwa mteja pamoja na mwongozo wa uwandaaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18.
Mafunzo hayo ya siku
tano yaliyoanza jana katika Ukumbi wa TBA mkoani Dodoma, yanashirikisha jumla
ya mikoa 19 yenye vituo vya TEMESA, yanatarajia kukamilika Ijumaa tarehe
20/01/2017. Aidha mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo kama hayo yaliyofanyika
mwezi Desemba, 2016 mkoani Dar es Salaam na yalishirikisha mikoa sita.
No comments:
Post a Comment