Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania Gao Wei
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kuhusu
maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaotarajiwa kuadhimishwa tarehe 21 na 22 mwezi huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yataambatana
na maonyesho ya utamaduni wa Kichina. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
HUAWEI Jimmy Liguo Jinna kulia ni Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya HUAWEI Jimmy Liguo
Jinna akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano
wa na waandishi hao kuhusu maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaotarajiwa kuadhimishwa
tarehe 21 na 22 mwezi huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina yatakayofanyika katika
viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 21 na 22 January 2017 kuanzia saa tatu asubuhi
mpaka saa 11 Jioni.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa China nchini Bw.Gao Wei
alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari.
Amesema mwaka huu
utafahamika kama mwaka wa Jogoo wenye kuweka mtazamo mkubwa Afrika huku
yakiambatana na burudani nyingi kutoka kwa vikundi mbalimbali vya sanaa kutoka
China na nchini,maonyesho ya picha,vyakula vya kichina na maonyesho mbalimbali
ya kibiashara.
Katika maadhimisho
hayo makampuni 60 yatashiriki katika kuonyesha bidhaa mbalimbali,pia nchi 150
na majiji 400 yatasherehekea maadhimisho haya ya mwaka mpya.
Akizungumzia
mahudhurio ya siku hiyo Bw.Wei amesema kuwa wanategemea ushiriki wa watu zaidi
ya 6000 katika maadhimisho hayo ya siku mbili ambayo yanasisitiza zaidi urafiki
na mshikamano.
Katika kufanikisha
maadhimisho hayo Kampuni za HUAWEI na CRDB Benki zimejitokeza kudhamini
maadhimisho ya mwaka huu.
No comments:
Post a Comment