Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, amezindua Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji wa
Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (Bus Rapid Transit - BRT) katika Kituo Kikuu
cha Mabasi kilichopo Kariakoo eneo la Gerezani jijini Dar es salam.
Uzunduzi huo
umehudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na
Somalia Bi. Bella Bird.
Awamu ya Kwanza ya
mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) yenye urefu wa
kilometa 20.9 unaojumuisha barabara ya Kimara – Kivukoni, Magomeni -
Morocco na Fire – Kariakoo ulikamilika Desemba 2015.
Aidha, utoaji wa
huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka ulianza tarehe 10 Mei, 2016. Kwa sasa huduma
ya mabasi katika kipindi cha mpito inatolewa katika njia nane, vituo vikuu
vitano, vituo vidogo 28 na karakana moja kwa kutumia mabasi 140 yanayojumuisha
mabasi makubwa 39 yenye uwezo wa kubeba abiria 160 kila moja na mabasi madogo
101 yenye uwezo wa kubeba abiria 60 kila moja.
Mradi wa ujenzi wa
Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) umepangwa kutekelezwa kwa awamu
sita kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment