Wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na
mkoani Geita wamelalamikia kitendo cha waendesha pikipiki pamoja na wafanyabiashara
ndogondogo katika mtaa wa Lutozo kuegesha pikipiki zao kando ya barabara jambo ambalo lina
hatarisha usalama wa watembea kwa miguu kutokana na kuwepo kwa msongamano uliokithiri.
Wakizungumza mapema hii leo kwa nyakati tofauti baadhi ya
wakazi wa eneo hilo wameiomba Serikali kupanua barabara hiyo ili iweze
kupunguza msongamano pia kuondoa adha
waipatayo watembea kwa miguu pindi watakapo kuvuka barabara hiyo kuelekea upande wa pili.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Jonathan Mchele amesema kuwa atashirikiana na jeshi
la polisi kikamilifu kuhakikisha
wanaliweka eneo hilo salama kwa watembea kwa miguu hasa wanafunzi.
Hata hivyo Diwani
wa kata hiyo ya katoro Bw. Benedect Kigongo amewataka wakazi wa eneo hilo kuwa
wavumilivu kwani suala hilo atalifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment