Mwenyekiti
wa chama cha wasanii Mkoani Geita,Rose Michael (ROSE BONANZA)akisoma risala
wakati wa ufunguzi wa mashindano ya wasanii wa maigizo na nyimbo mbele ya mgeni
rasmi kwenye ukumbi wa halmashauri ya mji wa Geita.
Chama cha wasanii Mkoani Geita,kimeiomba serikali Mkoani humo kuendelea
kutoa ushirikiano katika Nyanja hiyo muhimu ikiwa ni pamoja na kusapoti
kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na wasanii.
Kauli hiyo imesemwa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Humo Rose Michael
wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuwasaka wasanii wenye vipaji vya kuimba, kuigiza
na kuchekesha yaliyokuwa yanafanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Mji wa
Geita.
Bi.Rose alisema kuwa Tasnia ya sanaa bado inachangamoto nyingi ikiwa ni
pamojan na kushindwa kutambulika na kushikwa mkono kwenye serikali
kutokana na kwamba baadhi viongozi wa kiserikali wanaona swala la
wasanii limekaa kiunu jambo ambalo si kweli kwani kazi ya sanaa ni
sawa na shughuli zingine katika jamii.
“Sisi wasanii bado tunachangamoto kubwa sana katika serikali ingawa kwa
sasa kuna wizara inayotutambua lakini bado kuna ugumu mwingi tu tukiangali
kwenye serikali kuna viongozi ambao wanaona kuwa hatuna mchango wowote lakini
sio kweli sisi tunauwezo wa kufikisha ujumbe kwa jamii na ikatuelewa zaidi
kuliko vile ambavyo serikali imeendelea kutuchukulia”alisema Rose.
Kwa upande wake mwenyekiti wa waigizaji Mkoa wa Mwanza,Ramadhani Masululi,amesema
kuwa jambo ambalo limekuwa likisababisha sanaa au wasanii kuonekana ni wahuni
ni kutokana na baadhi ya wasanii kuonekana kutokujieshimu na wengine kuingia
kwenye sanaa bila ya kuwa na maono au mtazamo chanya katika sanaa.
“Sanaa sio uhuni kwanini wanasema uhuni waigizaji wengine wameingia
ni mamluki unakuta mwingine anaingia kwenye sanaa ni mlevi mvuta bangi na
mwingine ni Malaya na hii ya wezekana kwasababu nikutokana na vigezo kutokuwa
vigumu lakini sisi kama chama cha wasanii hatuwezi kukubaliana na
swala hili tutaakikisha wale wenyetabia za ajabu wanatupisha ili tuwe na
wasanii ambao wananidhamu”alisema Ramadhani
Akimwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita ambaye ndiye
alikuwa mgeni rasimi kwenye uzinduzi huo,afisa maendeleo ya jamii wa
halmashauri hiyo,Maiga Majagi,amewaasa wasanii kutumia umoja wao kuleta
mabadiliko kwa wanageita kwa kufanya kazi na kukitumia chama chao kwa kuwa
tetea zaidi na kupata taarifa mbali mbali za soko la kazi zao na pia
amewataka kupanga mikakati ya kushirikiana na wadau wote na
kwamba jambo likiongelewa na wote linakuwa na nguvu kuliko kuzungumziwa na mtu
mmoja.
No comments:
Post a Comment