KUHABARISHA NA KUFAHAMISHA KUHUSU HABARI NA MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII YA GEITA, KANDA YA ZIWA, TAIFA NA DUNIANI. TUTUMIE HABARI AU WASILIANA NASI KUPITIA info@stormfm.co.tz au +255 685 883 870
Monday, 30 January 2017
WALIMU SHULE YA MSINGI ISABILO WAGOMA KUFANYA KAZI
Walimu wa shule ya msingi Isabilo wilaya na Mkoa wa Geita wamegoma kufanya kazi tangu Januari 25 mwaka huu kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kukosa morali ya kazi baada ya wanakijiji kuvamia na kuwapiga walimu wawili kwa tuhuma za kuwaadhibu watoto wao.
WAHANGA 15 WALIOFUKIWA NA MGODI WA RZ WARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALINI LEO
Mchungaji wa Kanisa FPCT Geita
Mathias Gundula ,Akimshukuru Mungu juu ya yale ambayo ameyateda kwa
vijana ambao wameokolewa kutoka mgodini.
Mkuu wa
Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiwasalimia wachimbaji
ambao walikuwa wamefukiwa na kifusi kwenye Mgodi wa RZ,katika Hosptali ya Rufaa
ya Geita.
Wahanga 15
wakiwemo watanzania 14 na Raia mmoja wa kichina walionusurika na kifo baada ya kuokolewa kutoka chini ya ardhi
kwenye mgodi wa dhahabu wa RZ Union
ulioko kijiji cha Mawe-meru kata ya Nyarugusu mkoani Geita baada ya kukaa
siku 3 bila chakula wala huduma wameruhusiwa kutoka hospital ya mkoa wa geita
walikopelekwa kupata matibabu.
BALOZI OMBENI SEFUE ATEULIWA JOPO LA WATU MASHUHURI AFRIKA
Friday, 27 January 2017
KICHANGA CHATUPWA CHOONI MKOANI GEITA
SERIKALI YA KIJIJI CHA LWAMGASA HATIANI KUSHITAKIWA MAHAKAMANI
Mkuu wa
wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitoa maagizo wakati wa mkutano wa kusoma
mapato na matumizi uliofanyika kwenye kijiji cha Lwamgasa.
Mtendaji wa
kijiji cha Lwamgasa ,Samwel Shosha akisamo taarifa ya mapato na matumizi ya
kijiji.
Mkuu wa
wilaya pamoja na Diwani wa Kata ya Lwamgasa wakifatilia kwa makini taarifa ya
mapato na matumizi ya kijiji
Thursday, 26 January 2017
MA RC, DC WAAGIZWA KUHAKIKISHA WANACHUKUA HATUA DHIDI YA TATIZO LA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizindua kitabu cha Mwongozo
wa Taifa wa Utekelezaji wa Sera za Huduma kwa watoto waliokatika mazingira
hatarishi kwa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio
kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la
Marekani (USAID) nchini Tanzania Tim
Donnay, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Naibu Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt.
Zainab Chaula na Msaidizi wa Waziri wa Nchi TAMISEMI
RAIS MAGUFULI KUWA MGENI RASMI SIKU YA SHERIA NCHINI
Kaimu Jaji
Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akiongea na wanahabari (hawapo
pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika
hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Jaji
Kiongozi wa Mahakam Kuu Tanzania Jaji Ferdinandi Wambali (kushoto) akiongea na
wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria
nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo
jijini Dar es Salaam.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina Revocati akiongea na
wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria
nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo
jijini Dar es Salaam.
WATU 14 WAMEFUKIWA NA UDONGO KWENYE MGODI
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA KUKOSA HEWA NDANI YA KISIMA
SAKATA LA MAJERUHI WALIOPIGWA NA MCHINA MKOANI GEITA LACHUKUA SURA MPYA
Wednesday, 25 January 2017
PICHA:WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NORWAY LEO
Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza mmoja wa wataalam
walioambatana na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad
(watatu kulia) walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar Es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. sifuni Mchome (wapili kulia) akifafanua jambo
wakati wa kikao na Balozi wa Norway na ujumbe wake (hawapo pichani)
walipotembelea Wizara hiyo leo ili kujadili namna wataalam hao wanavyoweza kusaidia
kiteknolojia katika kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akiagana na Balozi wa Norway
nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad na ujumbe wake baada ya kumaliza kikaol
eo jijini Dar es salaam.
TMAA YAJIDHATITI KUKUSANYA MAPATO SEKTA YA MADINI
Kaimu
Mkuu wa Kitengo Cha Habari toka Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA) Mhandisi Yisambi Shiwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini
Dar es salaam kuhusu mafanikio ya wakala huo katika kipindi cha Julai-Desemba
2016 ikiwemo kufanikiwa kukusanya Bilioni 79.26 zilizolipwa Serikalini na
Kampuni za Madini kama kodi ya mapato. Kushoto ni Meneja Utafiti na Mipango wa Wakala huo Bw. Julius Moshi na
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya Madini Migodi Mikubwa, ya
Kati na Midogo Mhandisi Baraka Manyama.
Meneja
Utafiti na Mipango wa Wakala wa Ukaguzi wa
Madini Tanzania (TMAA) Bw. Julius Moshi akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa
na wakala huo katika kuhakikisha kuwa Serikali inakusanya mapato yote yanayotokana
na Madini.
Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya wakala huo kusimamia
vyema sekta ya madini ili iweze kulinufaisha Taifa. Kulia ni Meneja Utafiti na
MipangowaWakala waUkaguzi waMadini Tanzania (TMAA) Bw. Julius Moshi.
Baadhi
ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA) leo Jijini Dar es salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya
madini migodi mikubwa,ya kati na midogo Mhandisi Baraka Manyama akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu kupatikana kwa malipo ya mrabaha kutokana
na shughuli za uchenjuaji wa marudio kwa kutumia teknolojia ya VAT LEACHING. Kulia
ni Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza na kushoto ni Meneja Utafiti na Mipango Bw. Julius Moshi.
Kaimu Mkurugenzi wa ukaguzi wa hesabu za Kodi na fedha za Migodi Bw. Venance Bahati akieleza
kwa waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya wakala huo kukagua migodi yote na
kuhakikisha kuwa Kodi zote zinalipwa Serikalini kwa kuzingatia sheria na kanuni
zinazosimamia sekta ya madini , kulia ni Meneja wa uthamini
wa Madini Bw.George Kaseza na kushoto ni
Meneja Utafiti na Mipango Bw. Julius Moshi.
PICHA: RAIS MAGUFULI: JENGENI KITUO CHA DALADALA NA KUPAKI MAGARI MADOGO KIMARA MWISHO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili
katika kituo cha mabasi yaendayo haraka Kariakoo Gerezani alipoenda kuzindua
Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam leo.Kulia
ni Makamu wa Rais wa Benki ya Diunia kwa Ukanda wa Afrika Maktahar Diop
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia
mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza
leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo wakati wa hafla
ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam,
awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais _TAMISEMI George Boniphace Simbachawene akizungumza jambo
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka
Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop akizungumza wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es
Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya
kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga aakimtambulisha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine
Mahiga(aliyesimama) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za
Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwaongoza
viongozi na wananchi wa Dar es Salaam kuimba wimbo wa taifa wakati wa hafla ya
uzinduzi Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam
leo. Kutoka kulia ni Mbunge wa Ilala Mussa Zungu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar
es Salaam Ramadhan Madabida,Waziri wa OR – TAMISEMI George Simbachawene, Makamu
wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Mambo ya Nje Balozi
Augustine Mahiga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Baadhi ya wakazi wa
jiji la Dar es Salaam wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka awamu ya
kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitazama
jiwe la msingi mara baada ya kuzindua rasmi Miundombinu na Huduma za Mabasi
yaendayo Haraka awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia kwa Rais
ni Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili
kulia), akiwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe (katikati) na Makamu wa Rais wa Benki ya
Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop wakimwagilia maji mti uliopandwa kama
kumbukumbu za uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka Dar
es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana
mkono na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop wakati
wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka Dar es
Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akieenda
kumtumza msaani wa muziki Mrisho Mpoto na Banana Zoro wakati
wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na
Huduma za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam leo. Uzinduzi huo
umefanyika katika kituo cha mabasi yaendayo haraka cha Gerezani Kariakoo amba
Mpoto na Banana waklitumbuiza wimbo wao unaohamasisha wananchi kufanya kazi
hali iliyomvutia Rais Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha na
baadhi ya viongozi wa kiserikali na siasa wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka, awamu ya kwanza leo jijini Dar
es Salaam.Aliyemshikana naye mkono ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya
Mwita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha
Basi la Mwendokasi mara baada ya kuzindua Miundombinu na Huduma za Mabasi
yaendayo Haraka, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
SERIKALI YASITISHA KUPOKEA WAKIMBIZI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU
RAIS MAGUFULI AZINDUA MRADI WA MABASI YA MWENDO KASI LEO JIJINI DAR
Monday, 23 January 2017
RAIS WA UTURUKI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan aliyefuatana na
mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifuhia ngoma kwenye uwanja wa ndege
wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo kuwasili kwa
ziara rasmi nchini Januari 22, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo
kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Rais wa Uturuki
Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini jana jioni (Jumapili, Januari 22,
2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya
Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.
Rais huyo ameambatana
na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo
ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat
Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak
Pia Rais huyo
ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.
UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI NKOME WAMALIZIKA KWA USALAMA
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya kupiga kura kutoka kwa msimamizi
Askari polisi wakiimarisha ulinzi katika kituo cha kupigia kura
WATANZANIA WAHIMIZWA KUZINGATIA USAWA WA KIJINSIA KATIKA SEKTA YA KILIMO
Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mradi wa
uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo
UDSM Profesa Bertha Omari Koda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES
Dkt. Rose Kingamkono akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu
kinachotumika kutoa elimu juu ya usawa wa kijinsia katika sekta ya kilimo,
sheria za kimila leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mhadhiri wa Shule
Kuunya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) Bw. Dotto Kuhenga,
Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda
na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka
LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari
Koda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wao na
waandishi hao(hawapo pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia
katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam.Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’
LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala
Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Sehemu ya Uandishi wa Habari na
Mawasiliano ya umma –SJMC) Bw, Dotto Kuhenga akionyesha waandishi wa habari
kitabu cha mwongozo wa waandishi wa habari katika utekelezaji wa
mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na
lishe leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtafiti kutoka
Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda (kulia).
Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka
LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa
uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono.
Subscribe to:
Posts (Atom)