MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC leo watakuwa wanatafuta ushindi wa kwanza katika Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, watakapomenyana na Medeama ya Ghana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Huo utakuwa mchezo wa mwisho wa mzunguko
wa kwanza na wa tatu kwa washindi hao wa mataji yote Tanzania Bara, baada ya
awali kufungwa mechi mbili, moja ugenini na moja nyumbani.
Yanga ilianza kwa kuchapwa 1-0 na
Mouloudia Olympique Bejaia nchini Algeria kabla ya kufungwa 1-0 tena na TP
Mazembe ya DRC mjini Dar es Salaam.
Na leo timu ya kocha Mholanzi, Hans van
der Pluijm inacheza mechi ya pili mfululizo nyumbani ikisaka ushindi wa kwanza,
ili kurejesha matumaini ya kwenda Nusu Fainali.
Yanga ilianza kwa kuchapwa 1-0 na Mouloudia Olympique Bejaia nchini Algeria kabla ya kufungwa 1-0 tena na TP Mazembe ya DRC mjini Dar es Salaam.
Na leo timu ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm inacheza mechi ya pili mfululizo nyumbani ikisaka ushindi wa kwanza, ili kurejesha matumaini ya kwenda Nusu Fainali.
Yanga SC watapigania ushindi wa kwanza Kombe la
Shirikisho leo jioni
|
Kundi
A
Na
|
Timu
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
Pts
|
1
|
TP Mazembe
|
2
|
2
|
0
|
0
|
4
|
1
|
3
|
6
|
2
|
Mouloudia Bejaia
|
2
|
1
|
1
|
0
|
1
|
0
|
1
|
4
|
3
|
Medeama
|
2
|
0
|
1
|
1
|
1
|
3
|
-2
|
1
|
4
|
Yanga SC
|
2
|
0
|
0
|
2
|
0
|
2
|
-2
|
0
|
Kundi B
Na
|
Timu
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
Pts
|
1
|
Kawkab Marrakech
|
2
|
2
|
0
|
0
|
4
|
2
|
2
|
6
|
2
|
FUS Rabat
|
2
|
1
|
1
|
0
|
2
|
1
|
1
|
4
|
3
|
Etoile Sahel
|
2
|
0
|
1
|
1
|
2
|
3
|
-1
|
1
|
4
|
Al Ahly Tripoli
|
2
|
0
|
0
|
2
|
1
|
3
|
-2
|
0
|
Katika mchezo wa leo, Yanga itawakosa wachezaji wake watatu tegemeo, beki wa kushoto Mwinyi Hajji Mngwali, viungo Deus Kaseke na Geoffrey Mwashiuya ambao wote ni majeruhi.
Aidha, Yanga itaendelea kumkosa beki wake mpya wa kulia, Hassan Kessy ambaye klabu yake ya zamani, Simba SC imegoma kumuidhinisha achezee klabu mpya.
Mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe alikuwa anasumbuliwa na Malaria kwa wiki yote hii, lakini tangu juzi amefanya mazoezi kikamilifu na wenzake, kuashiria kwamba anaweza kucheza leo.
Medeama iliyowasili Alhamisi Dar es Salaam nayo haijashinda mechi baada ya kufungwa ugenini na TP Mazembe 3-1 na kulazimishwa sare ya 0-0 nyumbani na MO Bejaia.
Bejaia wanatarajiwa kucheza kwa kushambulia leo, kwa sababu pamoja na kucheza ugenini lakini wanahitaji kushinda leo ili kufufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali.
Kwa Yanga leo ni mtihani kweli kwa Pluijm aliyewahi kufundisha Medeama, kwani atahitaji kutafuta mabao na kujizuia kutoruhusu bao ili kukamilisha mpango wa kushinda mechi ya kwanza.
Mchezo mwingine wa kundi hilo utachezwa kesho,
Mouloudia Bejaia wakiikaribisha TP Mazembe Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia kuanzia Saa 3:45 usiku.
Mechi za Kundi B Kawkab Marrakech watakuwa wenyeji wa ndugu zao, FUS Rabat Uwanja wa Grand Marrakech, wakati Etoile Sahel wanaikaribisha Al Ahly Tripoli ya Libya leo Uwanja wa Olympique de Sousse, Tunisia.
No comments:
Post a Comment