Monday, 11 July 2016

WAKAZI WA KIJIJI CHA NKOME MKOANI GEITA WAKUMBANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA USAFIRI














Wananchi wanaotumia kivuko kilichopo  katika Kata na Kijiji cha Nkome wilayani na mkoani Geita kuvuka kuelekea sehemu tofauti wanalazimika kupita ndani ya maji kutokana na kivuko hicho kujaa maji hali ambayo imekuwa ikisababisha madhara kwa watumiaji   ikiwemo ajali na magonjwa mbalimbali.
Hayo yamebainishwa  na baadhi ya watumiaji wa daraja hilo walipokuwa wakizungumza na storm habari kivukoni hapo ambapo wamesema kuwa wamekuwa wakilazimika kupita ndani ya maji ili kuvifikia vyombo vya usafiri jambo ambalo limekuwa likiwasababishia ajali na magonjwa kutokana na kukanyanga  maji   hayo.

Wamesema kuwa licha ya kupata magonjwa na ajali, wanawake pia wamekuwa wakidhalilika kwani hulazimika kuvua nguo ili kuepuka kuloa na maji  jambo ambalo ni fedheha hata kwa watoto wadogo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata  ya  Nkome Bw.Michael Luyaga amesema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Geita  haina mafungu ya kuweza kusimamia suala hilo kwani vivuko vyote vimekuwa vikisimamiwa na wakala wa ufundi na umeme mkoni geita (TEMESA).


hata hivyo Kaimu Meneja wa TEMESA mkoani hapa mwandisi  Gile  Chacha amekiri kuitambua changamoto hiyo na kwamba amesema ujenzi wa kivuko hicho utaanza rasmi mara baada ya maji yaliyofunika daraja hilo kupungua kwani mikakati yote ikiwemo bajeti nzima imekwishakamilika huku akiwataka wananchi kuwa wavumilivu kwani jambo hilo linashughulikiwa. 

No comments:

Post a Comment