KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa anaondoka
leo Bathlehem kuhamia Johannesburg, Afrika Kusini kujiiunga na klabu mpya,
Moroka Swallows ya huko.
Moroka Swallows imeinunua Free State Stars ya Bethlehem na sasa kupata haki ya kushiriki tena Ligi Kuu ya Afrika ABSA Kusini.
Ngassa ameongea kwa simu leo kutoka Afrika Kusini kwamba mpango wa Free State kununuliwa na Swallows umekamilika na wachezaji wote wanahamia Johannesburg leo.
"Tunaondoka leo, tunahamia Moroka Swallows, mikataba
yenu inahamia kule na tumeambiwa tutatekelezewa haki zetu kama kawaida. Ndiyo
tunakwenda kuanza maisha mapya,”amesema.
Baada ya kushuka daraja kwa mara ya pili ndani ya misimu miwili, mwishoni mwa msimu wa 2015/2016, Swallows imefanikiwa kurejea Ligi Kuu kwa kuinunua Free State.
Baada ya kushuka daraja kwa mara ya pili ndani ya misimu miwili, mwishoni mwa msimu wa 2015/2016, Swallows imefanikiwa kurejea Ligi Kuu kwa kuinunua Free State.
Bodi ya Ligi ya PSL imebariki mpango huo baada ya kuufanyia tathmini na kujiridhisha kanuni zote zimefuatwa.
Stars inakuwa timu ya pili kuuzwa tangu mwishoni mwa msimu uliopita, baada ya Mpumalanga Black Aces kuuzwa kutoka kwa Mario na George Morfou kwenda kwa John Comitis - na sasa inajulikana kama Cape Town City FC chini ya mmiliki mpya.
Ngassa alijiunga na Free State Stars msimu uliopita kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Yanga na wakati anajiandaa kuingia katika msimu wake wa pili kwenye mkataba wa miaka minne, timu hiyo inataka kuuzwa.
No comments:
Post a Comment