BEKI wa Yanga, Juma Abdul Jaffar Mnyamani ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/2016.
Katika sherehe za utoaji wa tuzo hizo usiku huu ukumbi wa Double Tree Hotel By
Hilton, Masaki, Dar es Salaam, Abdul ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa,
Taifa Stars amewashinda beki mwenzake, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba
na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shizza Kichuya.
Na kwa ushindi huo, Abdul mbali na kukabidhiwa taji na mgeni rasmi, Waziri wa
Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, pia atazawadiwa fedha Sh Milioni 9.2 wakati
klabu yake, Yanga SC itazawadiwa Sh. Milioni 81.3 kwa kuwa bingwa, huku Sh. Milioni
40.6 zikienda kwa washindi wa pili, Azam FC, Sh Milioni 29 zikienda kwa
washindi wa tatu, Simba SC na Sh. Milioni 23.2 zikienda kwa Prisons washindi wa
nne.
Waziri wa Mambo ya
Ndani, Mwigulu Nchemba (kulia) akimkabidhi Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu,
Juma Abdul (kushoto) usiku huu hoteli ya Double Tree By Hilton
Rais wa TFF, Jamal
Malinzi akimkabidhi mfano wa Hundi, Thabani Kamusoko aliyeongozana na mkewe
Bongile Sibanda (kushoto) na mwanawe, Shanna Lee
Kipa bora wa zamani,
Mwameja Mohammed (kushoto) akimkabidhi tuzo ya Kipa Bora wa Ligi Kuu, Aishi
Manula (kulia)
Hans van der Pluim
akipunga mkono baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya Kocha Bora wa Ligi Kuu
Aishi Salum Manula wa Azam FC ameshinda tuzo ya kipa Bora akiwaangusha Deo
Munishi ‘Dida’ wa Yanga na Benno Kakolanya wa Prisons na kuzawadiwa Sh. Milioni
5.7 huku mfungaji bora Amissi Tambwe wa Yanga akizawadiwa pia Sh. Milioni 5.7.
Thabani Michael Kamusoko ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Kigeni,
akiwaangusha Mzimbabwe mwenzake anayecheza naye Yanga SC, Donald Ngoma na kipa
Muivory Coast wa Simba, Vincent Agban hivyo kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 pia.
Mholanzi Hans van der Pluijm ameshinda tuzo ya Kocha Bora na kuzawadiwa Sh.
Milioni 8, akiwaangusha Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar na Salum Mayanga wa
Prisons.
Tshabalala ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi akiwaangusha Farid Mussa
wa Azam na Shizza Kichuya wa Mtibwa Sugar na kuzawadiwa Sh. Milioni 4.
Ibrahim Hajib wa Simba ameshinda tuzo ya Bao Bora la Msimu na kuzawadiwa Sh.
Milioni 3 akimuangusha Tambwe wa Yanga, wakati Mtibwa Sugar imezibwaga JKT Ruvu
na Mgambo Shooting katika tuzo ya Timu yenye Nidhamu na kuzawadiwa Sh. Milioni
17.2.
Ngole Mwangole ameshinda tuzo ya Refa Bora na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 baada
ya kuwaangusha Anthony Kayombo na Rajab Mrope.
BEKI wa Yanga, Juma Abdul Jaffar Mnyamani ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/2016.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba (kulia) akimkabidhi Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, Juma Abdul (kushoto) usiku huu hoteli ya Double Tree By Hilton
Rais wa TFF, Jamal Malinzi akimkabidhi mfano wa Hundi, Thabani Kamusoko aliyeongozana na mkewe Bongile Sibanda (kushoto) na mwanawe, Shanna Lee
Kipa bora wa zamani, Mwameja Mohammed (kushoto) akimkabidhi tuzo ya Kipa Bora wa Ligi Kuu, Aishi Manula (kulia)
Hans van der Pluim akipunga mkono baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya Kocha Bora wa Ligi Kuu
Thabani Michael Kamusoko ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Kigeni, akiwaangusha Mzimbabwe mwenzake anayecheza naye Yanga SC, Donald Ngoma na kipa Muivory Coast wa Simba, Vincent Agban hivyo kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 pia.
Mholanzi Hans van der Pluijm ameshinda tuzo ya Kocha Bora na kuzawadiwa Sh. Milioni 8, akiwaangusha Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar na Salum Mayanga wa Prisons.
Tshabalala ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi akiwaangusha Farid Mussa wa Azam na Shizza Kichuya wa Mtibwa Sugar na kuzawadiwa Sh. Milioni 4.
Ibrahim Hajib wa Simba ameshinda tuzo ya Bao Bora la Msimu na kuzawadiwa Sh. Milioni 3 akimuangusha Tambwe wa Yanga, wakati Mtibwa Sugar imezibwaga JKT Ruvu na Mgambo Shooting katika tuzo ya Timu yenye Nidhamu na kuzawadiwa Sh. Milioni 17.2.
Ngole Mwangole ameshinda tuzo ya Refa Bora na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 baada ya kuwaangusha Anthony Kayombo na Rajab Mrope.
No comments:
Post a Comment