Hali ya sintofahamu juzi
Imewakumba wakazi wa Kijiji cha Ihumilo Kata ya Nkome wilaya na Mkoa wa Geita
baada ya mifupa ya binadamu anayedaiwa kuzikwa zaidi ya miaka 10 iliyopita
kuonekana kandokando ya Ziwa Victoria.
Mifupa hiyo iliyoonekana ikiwa
imehifadhiwa kwenye kipande cha karatasi ya plasitiki nyeusi ilionekana tangu
Julai 7 mwaka,katika mwalo wa Mchangani baada ya kaburi lake kufukuliwa na
mawimbi ya maji kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji ya Ziwa Victoria.
Mwenyekiti wa Kitongoji Cha
Mchangani Simoni Malole amesema mifupa hiyo ni ya mtu aliyezikwa kati ya
mwaka 2006 na 2007,baada ya kufa maji na mwili wake kuonekana ukielea juu ya
maji na alizikwa eneo hilo kwa kukosa ndugu.
Mifupa hiyo iliondolewa juzi na wananchi na kwenda kuzikwa eneo jingine baada ya mahakama ya Nyamboge Kutoa kibali kwa mujibu wa sheria na zoezi hilo kusimamiwa na askari polisi wa kituo kidogo cha Nkome chini ya Mkuu wake Inspekta Ndege.
Aidha Ofisa Mtendaji
wa Kijiji cha Ihumilo John Misango amewataka wananchi kuacha taboa ya
kuzika kandokando ya ziwa na badala yake wanapaswa kutunza mazingira ya ziwa
kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment