Bingwa
wa mbio za Olimpiki za walemavu Oscar Pistorius, kutoka Afrika Kusini,
amehukumiwa kufungwa jela miaka sita kwa kumuua mpenzi wake mwaka 2013.
Alikuwa amekabiliwa na uwezekano
wa kufungwa jela zaidi ya miaka 15.
Mawakili wa upande wa mashtaka na
wa upande wa mshtakiwa wanaweza kukata rufaa.
Uamuzi wa mahakama nchini
umetolewa baada ya kubatilishwa kwa hukumu ya awali ya kuua bila kukusudia kuwa
mauaji mwezi Desemba baada ya upande wa mashtaka kukata rufaa.
Pistorius, 29, alimpiga risasi
Reeva Steenkamp mara nne mnamo February 14 2013. Amepelekwa jela ya Khosi Mampuru mjini Pretoria.
No comments:
Post a Comment